Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watafahamu ya kuwa katika maisha yetu hata tunapopata shida Mungu yu tayari kutuongoza na kutulinda.
- Watamtegemea Mungu kwa maisha yao ili wakue ndani ya imani yao.
- Watamfuata Mungu ndani ya imani yao kwa sababu anawasindikiza pia kama alivyowasindikiza Waisraeli ndani ya safari yao.
+Maelezo juu ya somo
Sisi hatujajua kwa hahika kabisa Musa na Waisraeli walitumia njia gani mpaka mlima Sinai. Watalamu wanaongea kuhusu njia mbili tofauti. Ukiangalia mchoro wa ramani chini unaonyesha njia iliyokubaliwa na wengi.
Ni muhimu mwalimu awaonyeshe ramani hii au achore ubaoni.
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
Jumapili iliyopita tulijifunza kuhusu kuandaa kuhama au kusafiri. Leo tunapenda kuongea kuhusu kusafiri ama kuhama.
- Nani ameshasafiri kwa siku nyingi ama amehamia hapa?
- Mlikwenda wapi? Mlitoka wapi? (kuhama kutoka wapi?)
- Mlichukua vitu gani? Na vitu gani mliacha nyumbani au sehemu nyingine?
- Mlikaa wapi njiaani?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Wewe umeshasafiri au ulihamia hapahapa. Leo pia tunajifunza kuhusu watu kama millioni mbili waliohama Misri na nini kilichotokea katska afari yao. Maana leo wanaondoka kweli ndani ya somo letu na wanasafiri.
Simulizi
„Siku moja… Kutoka 13: 17 – 14: 31
Maneno magumu usimulie ndani ya simulizu, sehemu ya mwanzo zaidi. Uonyesha picha ya somo la leo!
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Mungu aliwaongoza Waisraeli kwa ishara gani wakati wa mchana na usiku walipotoka Misri?
- Waisraeli waliwafuata katika vyombo gani?
- Waisraeli walipata hofu gani na walimwambia Musa nini?
- Musa aliwapa faraja gani?
- Kwa njia gani Mungu aliwapitisha Waisreali katika bahari?
- Ilitokea nin kwa upande wa Wamisri waliowafuata?
Maelezo mafupi: Kweli Waisraeli walikumbuka ndani ya safari yao kwamba walipokaa Misri ilikuwa rahisi zaidi. Walisahau kwamba walipata maisha yamagumu kwa sababu waliona maisha ya jangwani ni magumu zaidi. Walichoka kutoka safari ndefu na hawajui wanaelekea wapi. Jangwa lipo nyuma yao na bahari ipo mbele. Hofu imezidi kuliku imani yao.
Pia sisi tukipata changamoto na shida ndani ya maisha yetu, tunafanya nini? Tunapata hofu au tunamtegemea Mungu zaidi? Hii ni swali kwetu leo.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Wanawaonyesha Mungu aliwaongoza Waisraeli kwa ishara gani kwa mchana na usiku walipotoka Misri?
- Waisraeli waliwafuata katika vyombo gani?
- Waisraeli walipata hofu gani na walimwambia Musa nini?
- Musa aliwapa faraja gani?
- Kwa njia gani Mungu aliwapitisha Waisreali katika bahari?
- Ilitokea nin kwa upande wa Wamisri waliowafuata?
Maelezo mafupi: Kweli Waisraeli walikumbuka ndani ya safari yao kwamba walipokaa Misri ilikuwa rahisi zaidi. Walisahau kwamba walipata maisha magumu kwa sababu waliona maisha sasa jangwani ni magumu zaidi. Walichoka kutoka safari ndefu na hawajui wanaelekea wapi. Jangwa li po nyuma yao na bahari ipo mbele. Hofu imezidi kuliku imani yao.
Pia sisi tukipata changamoto na shida ndani ya maisha yetu, tunafanya nini? Tunapata hofu au tunamtegemea Mungu zaidi? Hili ni swali letu leo. Ufikiri kwanza kwa ukimya kuhusu swali hili. Unafanya nini kama wewe ukipata changamoto au shida? Unapata hofu zaidi au unamtegemea Mungu?
Maigizo: Watoto wote kwa kikundi hiki pamoja na mwalimu wao au walimu wao wanaweza kuigiza wote somo hili kwa kutumia vitendo mbalimbali. Maana wote wanaigiza vitendo vyote. Mwalimu mmojawapo ni kiongozi kwa simulizi hili na anasimulia tena somo hili. Lakini vitendo pia na watoto wanafanya pamoja naye. Asubiri kidogo mpaka wote wamelewa igizo la aina hii:
- Wototo wajipange katika mistari ya wawili wawili na waanza kutembea kama wanajeshi lakini pia wabebe mizigo. (Kutoka 13:18)
- Baada ya muda wa kutembea watoto na walimu wasimame na wapumzike. Maana wanakaa chini na kuigiza kama wanaandaa chakula, kula chakula na kulala. (Kutoka 13: 20)
- Watoto wanaigiza sasa wingu na moto (Kutoka 13:21 na 22). „Wingu” wanalichora hewani na moto wanaweka mikono juu kama ulimi wa moto.
- Watoto wanarudi kidogo kwa njia yao lakini wanajipanga tena kwa mistari. Wanaenda sehemu nyingine kupumzika sasa. Wanapiga hema, wanaandaa chakula, kula na kulala. Wachache wanaigiza kama ni walinizi wa kampi hizi. (Kutoka 14: 1 – 4)
- Pia wote wanafanya kama wanamsikia Mungu kama Musa alivyomsikia Mungu. Wanamsikia ana mpango gani na Farao.
- Watoto wanaigiza sasa Farao. Huyu Farao anajiuliza kwa sababu gani walitoa ruhusa kwa Waisraeli kuondoka na sasa hamna watu kuwahudumia. (Kutoka 14: 5)
- Wanaendelea kuigiza na walimu: Farao na wanajeshi wengi waendesha sasa magari yenye farasi mbele. Wote wanafanya vitendo hivyo na wanaongeza mwendo. (Kutoka 14: 6 – 9)
- Watoto wanaigiza kama wanashangaza kwamba Farao na Wamisri wanawakaribia na wanaonyesha dalili ya hofu kuu! (Kutoka 14: 10)
- Halafu watoto wanaigiza kama wanamwuliza Musa na kulaumu kwa sababu wanapenda kurudi Misri na wanaona kubaki Misri ni bora kulika kukaa hapa hapa. Hawapendi kufariki jangwani. (Kutoka 14: 11 na 12)
- Musa anaongea nao na pamoja na mwalimu wanatumia maneno kutoka Biblia: “Msiogope, simameni tu, mwone wokovu wa Bwana atakaowafanyie leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya” (Kutoka 14:13 na 14)
- Wote wanafanya kama wanaweka fimbo juu. Watoto na walimu wanaonyesha ishara ya kugawa kitu katikati kama bahari imegawanika katikati. Na halafu wataanza kutembea katikati ya bahari. (Kutoka 14: 15 mpaka 18) Mwalimu pia anaendelea kusimulia.
- Watoto wanaigiza malaika na mabavu na kuchora hewani wingu. Waanaendelea kutembea katikati ya bahari bila shida. Lakini kama wakiigiza Wamisri wanatembea kama watu wasiooni. (Kutoka 14: 19 na 20).
- Musa anaweka mkono yake juu ya wanafanya sauti ya upepo na halafu wanatembea katikati ya bahari. Wanashangaa kuona ukuta upande wa kushoto na kulia. (Kutoka 14: 21 na 22)
- Wamisri wanawafuata kwa njia ya kuendesha gari lenye farasi. Lakini baada ya muda matairi yanakwama na watoto wanaigiza hii pamoja na hofu kuu kwa Wamisri: „Tutoroke! Mtorokeni!“ (Kutoka 14: 23 mpaka 25)
- Sasa Musa anaweka mkono wako juu tena na maji yanarudi. Pia wanaonyesha kwamba Wamisri sasa wanazama ndani ya maji! Watoto waigize vitendo hivi vitatu. (Kutoka 14: 26 – 28)
- Turudi kwa Waisraeli. Wao wanatembea bila shida na walipofika wanapiga magoti kumshukuru Mungu kwa utunzaji mkubwa sana. (Kutoka 14: 29 mpaka 31)
Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Mungu aliwaongoza Waisraeli kwa ishara gani wakati wa mchana na usiki walipotoka Misri?
- Waisraeli waliwafuata katika vyombo gani?
- Waisraeli walipata hofu gani na walimwambia Musa nini?
- Musa aliwapa faraja gani?
- Kwa njia gani Mungu aliwapitisha Waisreali katika bahari?
- Ilitokea nin kwa upande wa Wamisri waliowafuata?
Maelezo mafupi: Kweli Waisraeli walikumbuka ndani ya safari yao kwamba walipokaa Misri ilikuwa rahisi zaidi. Walisahau kwamba walipata maisha magumu kwa sababu waliona maisha sasa jangwani ni magumu zaidi. Walichoka kutoka safari ndefu na hawajui wanaelekea wapi. Jangwa lipo nyuma yao na bahari ipo mbele. Hofu imezidi kuliku imani yao.
Pia sisi tukipata changamoto na shida ndani ya maisha yetu, tunafanya nini? Tunapata hofu au tunamtegemea Mungu zaidi? Hili ni swali letu leo. Ufikiri kwa ukimya na uandike jibu lako kwa ukurasa mdogo ambao unapewa. Ujibu kwa ukweli!
Mwalimu awagawie karatasi ndogo ndogo kwa ajili ya kuandika na pia pen au pensili. Wachore pia ramani ya safari ya Waisraeli kutoka Misri.
Kama una muda unaweza kufanya maigizo na watoto wote.
Maigizo: Watoto wote kwa kikundi hiki pamoja na mwalimu wao au walimu wao wanaweza kuigiza wote somo hili kwa kutumia vitendo mbalimbali. Maana wote wanaigiza vitendo vyote. Mwalimu mmojawapo ni kiongozi kwa simulizi hili na anasimulia tena somo hili. Lakini anawaonyesha vitendo pia na watoto wanafanya pamoja naye. Asubiri kidogo mpaka wote wamelewa igizo la aina hii:
- Wototo wajipange katika mistari ya wawili wawili na waanza kutembea kama wanajeshi lakini pia wabebe mizigo. (Kutoka 13:18)
- Baada ya muda wa kutembea watoto na walimu wasimame na wapumzike. Maana wanakaa chini na kuigiza kama wanaandaa chakula, kula chakula na kulala. (Kutoka 13: 20)
- Watoto wanaigiza sasa wingu na moto (Kutoka 13:21 na 22). „Wingu” wanalichora hewani na moto wanaweka mikono juu kama ulimi wa moto.
- Watoto wanarudi kidogo kwa njia yao lakini wanajipanga tena kwa mistari. Wanaenda sehemu nyingine kupumzika sasa. Wanapiga hema, wanaandaa chakula, kula na kulala. Wachache wanaigiza kama ni walinizi wa kampi hizi. (Kutoka 14: 1 – 4)
- Pia wote wanafanya kama wanamsikia Mungu kama Musa alivyomsikia Mungu. Wanamsikia ana mpango gani na Farao.
- Watoto wanaigiza sasa Farao. Huyu Farao anajiuliza kwa sababu gani walitoa ruhusa kwa Waisraeli kuondoka na sasa hamna watu kuwahudumia. (Kutoka 14: 5)
- Wanaendelea kuigiza na walimu: Farao na wanajeshi wengi waendesha sasa magari yenye farasi mbele. Wote wanafanya vitendo hivyo na wanaongeza mwendo. (Kutoka 14: 6 – 9)
- Watoto wanaigiza kama wanashangaza kwamba Farao na Wamisri wanawakaribia na wanaonyesha dalili ya hofu kuu! (Kutoka 14: 10)
- Halafu watoto wanaigiza kama wanamwuliza Musa na kulaumu kwa sababu wanapenda kurudi Misri na wanaona kubaki Misri ni bora kulika kukaa hapa hapa. Hawapendi kufariki jangwani. (Kutoka 14: 11 na 12)
- Musa anaongea nao na pamoja na mwalimu wanatumia maneno kutoka Biblia: “Msiogope, simameni tu, mwone wokovu wa Bwana atakaowafanyie leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya” (Kutoka 14:13 na 14)
- Wote wanafanya kama wanaweka fimbo juu. Watoto na walimu wanaonyesha ishara ya kugawa kitu katikati kama bahari imegawanika katikati. Na halafu wataanza kutembea katikati ya bahari. (Kutoka 14: 15 mpaka 18) Mwalimu pia anaendelea kusimulia.
- Watoto wanaigiza malaika na mabavu na kuchora hewani wingu. Waanaendelea kutembea katikati ya bahari bila shida. Lakini kama wakiigiza Wamisri wanatembea kama watu wasiooni. (Kutoka 14: 19 na 20).
- Musa anaweka mkono yake juu ya wanafanya sauti ya upepo na halafu wanatembea katikati ya bahari. Wanashangaa kuona ukuta upande wa kushoto na kulia. (Kutoka 14: 21 na 22)
- Wamisri wanawafuata kwa njia ya kuendesha gari lenye farasi. Lakini baada ya muda matairi yanakwama na watoto wanaigiza hii pamoja na hofu kuu kwa Wamisri: „Tutoroke! Mtorokeni!“ (Kutoka 14: 23 mpaka 25)
- Sasa Musa anaweka mkono wako juu tena na maji yanarudi. Pia wanaonyesha kwamba Wamisri sasa wanazama ndani ya maji! Watoto waigize vitendo hivi vitatu. (Kutoka 14: 26 – 28)
- Turudi kwa Waisraeli. Wao wanatembea bila shida na walipofika wanapiga magoti kumshukuru Mungu kwa utunzaji mkubwa sana. (Kutoka 14: 29 mpaka 31)
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Zaburi 106:10 na unasema: “Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, na kuwakomboa na mkono wa adui zao”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Nani alimwokoa nani? Au nani aliwaokoa Waisraeli?
- Mungu alitumia kitu gani kuwaokoa?
- Mungu aliwaokoa na kuwakomboa kwa nani?
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kupita ishara zinazoelezwa.
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Zaburi 106:10 na unasema: “Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, na kuwakomboa na mkono wa adui zao”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Nani alimwokoa nani? Au nani aliwaokoa Waisraeli?
- Mungu alitumia kitu gani kuwaokoa?
- Mungu aliwaokoa na kuwakomboa kwa nani?
- Unafikiri katika siku hizi pamoja na maisha yetu nani ni adui yetu? Tunaweza kufanya nini na maadui zetu?
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Zaburi 106:10 na unasema: “Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, na kuwakomboa na mkono wa adui zao”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Nani alimwokoa nani? Au nani aliwaokoa Waisraeli?
- Mungu alitumia kitu gani kuwaokoa?
- Mungu aliwaokoa na kuwakomboa kwa nani?
- Unafikiri katika siku hizi na maisha yetu nani ni adui yetu? Tunaweza kufanya nini na maadui zetu?
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Baadaye wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na masomo haya. Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto watafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).