Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watafahamu kuwa Mungu amekwisha tayarisha njia ya kuwaokoa wanaomwamini.
- Wataelewa kwamba maana ya Pesach (kiebrania) ni “kupita juu ya” au “kuruka juu ja”.
- Wataweza kutofautisha Pesach, sherehe ya Wayahudi na Passaka, sherehe ya Wakristo.
Maelezo juu ya somo
Pigo la mwisho ilikuwa kifo cha wazaliwa wa kwanza kwa wanadamu na wanyama katika nchi ya Misri. Huzuni kubwa imikaa katikati ya Wamisiri na wote waliofiwa na mtoto wa kiume wa kwanza.
Pia Waisraeli wameambiwa kuwachinja kondoo au mbuzi kwa mwaka moja na kumchoma. Kutoka damu ya kondoo au mbuzi ni lazima waache kidogo kwa ajili ya kupaka sehemu tatu ya fremu ya mlango: kushoto na kulia na juu. Alama hii inawazuia na kifo. Malaika na Mungu mwenyewe akipita kwa usiku unaofuata anajua nani anayemwamini kwa alama hii ya damu.
Wazo lingine limeingia sasa utamaduni wa Wayahudi. Hii damu ya kondoo au mbuzi itakuwa na maana nyingine. Mungu aliwazuia kwa sababu damu ya kondoo (au mbuzi) zimepakwa fremu za milango na damu hii ya kondoo zimeleta wokovu kwa Waisraeli kipindi kile.
Pia sisi Wakristo tunasema Yesu Kristo aliyesulubishwa msalabani ni kama kondoo na damu yake imeleta wokovu kwa sisi Wakristo. Kwa hiyo tunasema damu ya Yesu Kristo aliyesulubishwa msalabani.
Maana ya Pesach ni “kupita juu ya” au “kuruka juu ya”. Kwa matukio haya inamaanisha kwamba Mungu amepita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kuangalia kwamba wanaomwamini wameweka alama za damu au hapana. Kama hawakuweka alimwua mtoto wa kwanza wa kiume.
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
Marudio:
- Waisraeli katika nchi ya Misri walikuwa na shida gani?
- Mungu aliwatuma watu gani ili awaokoe Waisareli?
- Farao alifanya nini aliposikia ujumbe wa Mungu?
- Mapigo tisa yalipita na Farao alikuwa na moyo wa namna gani?
Maswali ya utangulizi
- Nani amewahi kuandaa safari au kuhama?
- Ukiandaa safari unahitaji kuandaa nini?
- Ukihama unahitaji kufikiri kuhusu maandalizi gani?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Leo tunajifunza kuhusu watu kama millioni mbili walioandaa kuondoka Misri na nini ilichotokea kabla ya uhamaji wao na walihitaji kuandaa nini kwa safari yao kutoka Mungu.
+Simulizi
Siku moja… Kutoka 11: 4 – 6 na 12: 1 – 42: Unasimulia maelezo ya „Pesah“ ndani ya simulizi, mwanzoni. Pia uonyeshe picha ya somo la leo.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Pigo la kumi na la mwisho lilikuwa la namna gani?
- Farao aliwakubali sasa Haruni na Musa baada ya kifo cha mtoto wake wa kwanza?
- Waisraeli waliandaa mkate wa aina gani?
- Kondoo au mbuzi walichinjwa. Waisraeli walifanya nini na damu zilizobakizwa?
- Kwa nini walipaka damu katika fremu za milango?
Maelezo mafupi: Mungu alipita nyumba zenye alama ya damu. Kwa hiyo Waisraeli na waliomwamini walipata wokovu. „Kupita juu ya“ hii kwa lugha ya kiebrania ni „pesach“. Wayahudi wanakumbuka mpaka leo Mungu alifanya nini kwa usiku huu na wanasherekea sherehe ya Pesach. Na sisi Wakristo tunashereke Pasaka kwa sababu kifo cha Yesu kwa ajili yetu.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Pigo la kumi na la mwisho lilikuwa la namna gani?
- Waliandaa nini wakati wa safari ya kuhama Misri? Mungu aliwaambia kufanya aina gani ya maandalizi?
- Waisraeli waliokolewa kwa njia gani?
- Neno la “pesach” ni kiebrania na ina maana gani?
- Kwa nini Wayahudi wanasherekea sherehe ya „Pesach“ mpaka leo?
- Walichinja kondoo au mbuzi. Damu ya kondoo zimetumika na pia sisi leo tunaongea kuhusu mwana-kondoo. Mwana-kondoo yule anatukumbusha juu ya nani?
- Je, sisi Wakristo tunakumbuka wokovu wa Kristo kwa njia gani?
Maelezo mafupi: Mungu alipita nyumba zenye alama ya damu. Kwa hiyo Waisraeli na waliomwamini walipata wokovu. „Kupita juu ya“ hii kwa lugha ya kiebrania ni „pesach“. Uchore mlango na fremu yake. Halafu uchore na kupaka „damu“ ndani ya fremu upande wa kushoto, kulia na juu ya mlango.
Wayahudi wanakumbuka mpaka leo Mungu alifanya nini usiku huu na wanasherekea sherehe ya Pesach.
Na sisi Wakristo tunashereka Pasaka kwa sababu ya kifo cha Yesu kwa ajili yetu. Uchore tena mlango wa pili. Mbele ya mlango uchore msalaba.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Pigo la kumi na la mwisho lilikuwa la namna gani?
- Waliandaa nini kwa safari ya kuhama Misri? Mungu aliwaambia kufanya aina gani ya maandalizi?
- Waisraeli waliokolewa kwa njia gani?
- Neno la “pesach” ni kiebrania na lina maana gani?
- Kwa nini Wayahudi wanasherekea sherehe ya „Pesach“ mpaka leo?
- Walichinja kondoo au mbuzi. Damu ya kondoo imetumika na pia sisi leo tunaongea kuhusu mwana-kondoo. Mwana-kondoo yule anatukumbusha juu ya nani?
- Je, sisi Wakristo tunakumbuka wokovu wa Kristo kwa njia gani?
Maelezo mafupi: Mungu alipita nyumba zenye alama ya damu. Kwa hiyo Waisraeli na waliomwamini walipata wokovu. „Kupita juu ya“ hii kwa lugha ya kiebrania ni „pesach“. Uchore mlango na fremu yake. Halafu uchore na kupaka „damu“ ndani ya fremu upande wa kushoto, kulia na juu ya mlango.
Wayahudi wanakumbuka mpaka leo Mungu alifanya nini kwa usiku huu na wanasherekea sherehe ya Pesach.
Na sisi Wakristo tunashereka Pasaka kwa sababu ya kifo cha Yesu kwa ajili yetu. Uchore tena mlango wa pili. Mbele ya mlango uchore msalaba.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha 1 Wakorintho 5:7b na unasema: “Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Kila mwaka tunasherekea “Pasaka”. Tunakumbuka nini kuhusu Yesu?
- Kwa nini Yesu alikufa?
- Jina lingine kwa Yesu ni jina gani?
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo.
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha 1 Wakorintho 5:7b na unasema: “Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati:
- Kwa nini tunasema „Pasaka wetu amekwisha“?
- Nani amekuwa tayari kutolewa kuwa sadaka?
- Kristo alifanya nini kwetu?
- Tofauti ya sherehe ya „Pesach“, sherehe ya Wayahudi na „Passaka“, sherehe ya Wakristo ni nini?
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha 1 Wakorintho 5:7b na 5: 8 na unasema: “Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo . Basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyofichika, ndio weupe wa moyo na kweli.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati:
- Kwa nini tunasema „Pasaka wetu amekwisha“?
- Nani amekuwa tayari kutolewa kuwa sadaka?
- Kristo alifanya nini kwetu?
- Tofauti ya sherehe ya „Pesach“, sherehe ya Wayahudi na „Passaka“, sherehe ya Wakristo ni nini?
- Kwa nini sisi tunashauriwa katika Biblia kwamba tutoe chachu ya kale na chachu ya uovu na ubaya?
- Kwa nini Paulo anapenda sisi Wakristo tuwe weupe na moyo na kweli?
- Tukilinganisha chakula cha sherehe ya Wayahudi “Pesach” na chakula cha Bwana siku hizi tunaweza kusema nini? Tukumbuke Mbungu aliwaambia Musa na Haruni nini kipindi kile na tunatumia njia gani kushiriki Chakula cha Bwana.
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Baadaye wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na masomo haya. Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto watafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisi kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).