Picha

Utambulisho wa Deodatius Dominick Lyimo
Naitwa Deodatius Dominick Lyimo na sasa ninaishi Morogoro mjini. Mimi ni mzwalimwa wa mkoa wa Kilimanjaro, Moshi.

Kwa umri mimi nina miaka 48 na elimu yangu ni ya Sekondari, kidato cha nne.

Nilipomaliza kidato cha nne nilikwenda moja kwa moja kujifunza uchoraji zaidi, lakini tangu darasa la tatu nilikuwa na kipaji cha uchoraji. Nilichora katika karatasi za kawaida (daftarini) na penseli yenye rangi na baadaye nilijiunga na kikndi ambacho walikuwa na kufanya kazi ya uchoraji kwa ajili ya biashara. Nilijifunza ndani ya kikundi hiki Arusha jinsi ya kutumia rangi ya maji, rangi kwa ajili ya batiki na rangi za mafuta kwenye kanwas.
Ninachora picha za kitambaduni, picha za portrait, picha za wanyama, watu na aina nyingine kama abstract. Pia ninachora picha za dini za kikristo. Nina uwezo wa kuchora picha katika umbo ya dogo na hata kubwa zaidi kama utukutani.
Watoto wangu na mke wangu wanaishi kutokana na kipato cha kazi yangu cha uchoraji.

Kwa kazi hii ya kuchora picha za Biblia nimejifunza mambo mapya kuhusu Biblia na niantumaini kwamba watoto wanaoziona picha zangu watalielewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Nakutakia mafanikio zaida na kunapoendelea kujifunaz Shule ya Jumapili.

Ubarikiwe!

Deodatius Dominick Lyimo

Maonyesho ya picha za masomo ya Biblia