Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watajifunza kuwa Mungu hutoa kwa mahitaji ya watu wake wanaomtegemea katika maisha yao.
- Watatamani kwamba Mungu anawalinda wanaomwamini na anawapa riziki ya kila siku.
- Watafurahi na kumshukuru Mungu kwa mambo ambayo Mungu anawapa kila siku.
Tukiangalia masomo yetu tunagundua ni hadithi tatu. Waisraeli wamekosa maji ya kunywa na chakula cha kula. Wanalaumu na baada ya Musa alipoongea na Mungu wanapata maji safi ya kunywa na chakula cha kutosha kwa kila siku.
“Man hu?” maneno ya kiebrania yana maanisha “Nini hiki?. Waisreali walishangaa kuhusu aina ya “mkate” waliouona kila asubuhi. Maneno haya “man hu?” ni msingi wa neno la “manna”.
Waisraeli walipewa maji ya kunywa na maji matamu, pia walipewa kila asubuhi manna na kware kwa jioni. Mungu aliwapa chakula cha kutosha kila siku na alipenda wajifunze kumwamini kwamba anawapa chakula cha kutosha na maji matamu kwa kila siku. Lita mbili kwa manna zinatosha kwa kila siku kula.
Pia tunaweza kuona uhusiano na maji matumu na maneno ya Yesu yanayoandikwa Biblia kwamba yeye ni “maji ya uzima”. Lakini pia tunaona hii katika “manna” na mkate kwa Agana Jipya. Yesu anasema yeye ni “chakula/mkate wa uhai”.
Waisraeli walitembea miaka 40 sehemu ya jangwani kwa ajili ya kufika katika nchi yenye maziwa na asali.
Masomo haya matatu yametokea kama mwezi mmoja baada ya kuondoka na sisi tunaweza kugundua kwamba wameishiwa na chakula na hasa maji ya kunywa. Wamesahau Mungu aliwafanyia nini wakati wa nyuma na bado hawajaweza kumwamini Mungu asilimia 100. Lakini ni aina ya wanadamu. Au wameshazoea sana Mungu anawasaidia kwa kila kitu.
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
Jumapili zilizopita tumesikia masomo kuhusu kuandaa safari ya kuondoka Misri kwa sababu Waisraeli walifanya kazi kali ya utumwa na siku za kwanza za safari na nini kilichowatokea wao. Leo tunasikia somo la mwisho kuhusu safari hii.
Kabla ya kuanza kusikia somo jipya tunajibu tena maswali matatu:
- Nani ameshawahi kuumwa na njaa au kiu?
- Ukiumwa na njaa inakuwaje?
- Ukiumwa na njaa unapata changamoto gani kwa mwilini, mawazoni na hisia?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Tumefikiri kuhusu kuumwa na njaa na kiu na changamoto zake kama tukipata njaa na kiu. Leo pia tunajifunza kuhusu taifa moja ambalo wameumwa sana na njaa na wamepata sana shida ya kiu. Musa alitatua shida hizi kwa njia gani na kitu gani kilichotokea tunasikia sasa.
Simulizi
„Siku moja…“ Kutoka 15: 22 – 27, Kutoka 16: 1 – 15 na Kutoka 17: 1 – 7; Maneno magumu usimulie ndani ya simulizu, sehemu ya mwanzo zaidi. Uonyeshe picha ya somo la leo!
Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Waisraeli walitembea siku tatu bila maji ya kunywa. Wamemlaumu Mungu aliwasaidia kwa njia gani kupata maji matamu?
- Baada ya mwezi mmoja walipata njaa sana kwa sababu akiba ya vyakula vimeisha. Je, waliwamwmbia Musa nini?
- Musa aliongea na Mungu na Mungu alifanya nini asubuhi na jioni kuwalisha Waisreali?
- Musa aliwambia waokote manna kiasi gani?
- Waliendelea na safari. Walipata kiuo tena. Musa alifanya nini kwa msaada wa Mungu?
Maelezo mafupi: Waisreali hawakuona Mungu alifanya nini kila siku. Hawakumwamini Mungu kwamba amewasaidia kwa kila shida mpaka hapa hapa. Lakini Mungu anaendelea kuwatamani watu wake na kuwasaidia mpaka leo. Upendo na neema yake ni mkubwa sana.
Labda uimbe wimbo wa „Upendo wa Mungu ni mkubwa!“
Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Baada ya siku chache waisraeli walianza kunung’unika. Kwa sababu gani?
- Je, nani alikuwa na imani ndani ya somo hili?
- Mungu aliwasaidia kwa njia gani?
- Waisraeli waliishiwa na chakula baada ya mwezi moja na safari yao. Walifanya nini?
- Kosa lao lilikuwa nini?
- Mungu alipenda kuwafundisha watu hawa jambo gani?
- Waisraeli walipata shida mara tatu. Walifanya nini tena?
- Ingawa waisraeli waliona matendo ya Mungu tena na tena wanasahau kuamba awatunze na awalinde vizuri. Unafikiri kwa sababu gani?
Maelezo mafupi: Kweli Waisraeli walikuwa wagumu kuelewa mafundisho kutoka Mungu. Aliwasaidia tena na tena kutoka mapigo kumi katika Misri. Walisahau tena na tena kwamba yeye anaendelea kuwatunza na kuwalinda. Lakini Mungu anaona pia mpaka wanadamu wanaweza kukumwamini inachukua muda mrefu. Watu wanahita kupita mapito mengi na shida nyingi. Wakijifunza kwamba kuona Mungu anawafanyia nini, wanaanza kumwaini zaidi kukuamini, kumsifu na kumshukuru.
Je, wewe unaweza kumshukuru Mungu kwa mambo gani ndani ya maisha yako? Ongeeni ndani ya kikundi chenye watoto watano!
Tukusanye mawazo yetu!
Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12

+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Kutoka 3: 12a na unasema: “Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe!”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Mungu alionyesha kwa njia gani kwamba anakaa karibu nao?
- Anapenda kuwa karibu nawe pia. Unaweza kugundua kwa mambo gani?
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kupitia kuimba maneno haya. Untunge sauti kwa maneno haya!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka masomo yote yanayouhusiana na masomo ya Musa:
Tufanye marudio ya mistori yote ya moyo.
Somo la kwanza: Mtoto Musa: Mstari wa moyo wa kwanza ni kutoka ktiabu cha Zaburi 50: 15 na unasema: “Ukaniite siku ya mateso, nitakukuokoa, na wewe utanitukuza!” Uandike mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la pili: Musa, mkuu wa Misri: Mstari wa moyo wa pili ni kutoka kitabu cha Hesabu 32:23 na unasema: “… nanyi jueni kwamba hiyo dhambi yenu itawapata hapana budi.” Uandike mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la tatu: Musa huko Midiani: Mstari wa moyo wa tatu ni kutoka kitabu cha Kutoka 3:12a: “… bila shaka mim nitakuwa pamoja nawe!” Uandkie mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la nne: Musa mjumbe wa Mungu: Mstari wa moyo wa nne ni kutoka kitabu cha Zaburi 95:3: “kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, na mfalme mkuu juu ya miungu yote!” Uandikie mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la tano: Pasaka ya Bwana: Mstari wa moyo wa tano ni kutoka kitabu cha 1 Wokorintho 5: 7b “…. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.” Uandikie mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la sita: Kutoka kwa Waisreali: Mstari wa moyo wa sita ni kutoka kitabu cha Zaburi 106: 10: “Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, na kuwakomboa na mkono wa adui zao.” Uandike mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la saba tunafikiri pamoja mstari gani kutoka mistari hii sita unafaa sana na zaidi.
- Unafikiri mstari gani kutoka mistari hii sita unafaa zaidi kwa somo la leo kuwa kwa ajili ya mstari wa moyo ? Kwa sababu gani?
- Tukiangalia mistari yote tunaweza kukumbuka mambo gani ndani ya masomo yote ya Musa? Watoto wasimulie!
Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baada ya hii wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha moja inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka masomo yote yanayouhusiana na masomo ya Musa:
Tufanye marudio ya mistori yote ya moyo.
Somo la kwanza: Mtoto Musa: Mstari wa moyo wa kwanza ni kutoka kitabu cha Zaburi 50: 15 na unasema: “Ukaniite siku ya mateso, nitakukuokoa, na wewe utanitukuza!” Uandike mstari huu ubaoni baadaya kutajwa!
Somo la pili: Musa, mkuu wa Misri: Mstari wa moyo wa pili ni kutoka kitabu cha Hesabu 32:23 na unasema: “… nanyi jueni kwamba hiyo dhambi yenu itawapata hapana budi.” Uandike mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la tatu: Musa huko Midiani: Mstari wa moyo wa tatu ni kutoka kitabu cha Kutoka 3:12a: “… bila shaka mim nitakuwa pamoja nawe!” Uandkie mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la nne: Musa mjumbe wa Mungu: Mstari wa moyo wa nne ni kutoka kitabu cha Zaburi 95:3: “kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, na mfalme mkuu juu ya miungu yote!” Uandikie mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la tano: Pasaka ya Bwana: Mstari wa moyo wa tano ni kutoka 1 Wokorintho 5: 7b “…. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.” Uandikie mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la sita: Kutoka kwa Waisreali: Mstari wa moyo wa sita ni kutoka Zaburi 106: 10: “Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, na kuwakomboa na mkono wa adui zao.” Uandike mstari huu ubaoni baada ya kutajwa!
Somo la saba tunafikiri pamoja mstari gani kutoka mistari hii sita unafaa sana na zaidi.
- Unafikiri mstari gani kutoka mistari hii sita inafaa zaidi kuwa kwa mstari wa moyo kwa somo la leo? Kwa sababu gani
- Tukiangalia mistari yote tunaweza kukumbuka mambo gani ndani ya masomo yote ya Musa? Watoto wasimulie!
4. Watoto wa umri mkubwa wakariri mstari wa moyo. Baada ya hii wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha moja inayofuata chini ya maandiko au nyuma katika ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na masomo haya. Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto watafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisi kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
MAIGIZO: Watoto wanaigiza ishara fulani kwa kila somo:
- Somo la kwanza: Mtoto Musa => kumtuliza mtoto
- Somo la pili: Musa, mkuu wa Misri => kumwua mtu
- Somo la tatu: Musa, huko Midiani => kupiga magoti
- Somo la nne: Musa mjumbe wa Mungu => kusimama kwenye kujiamini
- Somo la tano: Pasaka ya Bwana => kupaka damu kwa pande zote tatu ya fremu ya mlango
- Somo la sita: Kutoka kwa Waisraeli => Kutembea na kubeba mizigo mizito
- Somo la saba: Safari mpaka Sinai => kuchuma manna na kunywa maji safi
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).