+Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watafahamu Mungu hutimiza makusudi yake kwa mikono ya watu wanaomtegemea waitikie wito wa Mungu katika maisha yao.
- Wataangalia mambo mawili ndani ya mazungumzo ya Mungu na Musa: Musa amejaribu kukataa kazi ngumu kutoka kwa Mungu, lakini Mungu alitoa moyo kwa njia ya kumsikiliza na kutoa ahadi.
- Watapata moyo kwamba Mungu anatupa sisi pia watu kutusaidia ndani ya kazi ngumu na maisha magumu kama mama, baba, dada, kaka, mjomba, jirani n.k.
+Maelezo juu ya somo
Musa alifanya kazi miaka arobaini kwenye jangwa la Sinai. Alijua sehemu na eneo kubwa vizuri sana kwa sababu alifanya kazi mchungaji wa baba mkwe wake. Mungu alimwita kipindi hiki misheni yake.
Maelezo yenyewe kuhusu wito ni mafupi, lakini tunapata taarifa muhimu: kitambulisho cha yule anayeita na kile Musa atachofanya. Mungu alimwita sehemu ya mlima wa Horebu. Mlima Horebu ni sawa na mlima Sinai. Ni majina mawili kwa mlima mmoja tu na ni mlima ule ule.
Mungu alimwambia Musa arudi Misri. Mahali ambapo Musa alikosa sana na mahali penye kumbukumbu mbaya kwa Musa. Aliposhindwa pale na ukiangalia mazungumzo kati ya Mungu na Musa unaweza kuona Musa hapendi kabisa kurudi Misri. Anajaribu kutoroka kazi na maigizo yake kwa njia tano, lakini Mungu anatoa mojo kwa Musa. Maigizo na kazi anazopewa kutoka Mungu kwa Musa ni kubwa sana pamoja na wajibu. Leo anaelewa maana ya kuwakomboa Waebrania na wenzake kutoka utumwa wa Farao na anajua hawezi kufanya hii bila msaada. Lakini miaka 40 iliopita alijiamini sana na alifikiri anaweza kufanya mwenyewe bila msaada wa Mungu. Kwa hiyo alijifunza kwamba hataweza kufanya bila msaada wa Mungu au mtu na ana mashaka na analeta pingamizi tano kwa Mungu na Musa anapokea majibu matano pia:
- „Je, mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikiwatoa wana wa Israeli watoke Misri?“ (Kutoka 3, 11)
- Mungu anamjibu „Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe, na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu. (Kutoka 3,12)
2. „Mungu, tazama, nitakapofika kwa wana wa Isreali, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, „Jina lake n’nani?“ Niwaambie nini? (Kutoka 3, 13)
- Mungu anamwambia: „Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; ndivyo utakavyowaambia wana wa Isreali; MIMI NIKO amenituma kwenu.“ (Kutoka 3, 14)
3. „Lakini Waisraeli hawataniamini wala kunisikiliza, bali watasema kuwa wewe Mwenyezi-Mungu hukunitokea“ Musa anajaribu mara ya tatu. (Kutoka 4:1)
- Mungu anamjibu tena kwa mifano miwili. Mfano wa fimbo ambayo inakuwa nyoka na imerudi kwa fimbo tena na mfano wa mkono mwenye ukoma. (Kutoka 4: 2 – 9)
4. Musa bado hajapenda kukubali na maigizo kutoka Mungu: „Ewe Bwana wangu, mimi sina ufusaha wa kuongea tangu zamani; hata baada ya wewe kusema nami mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito.“ (Kutoka 4: 10)
- Mungu anamwuliza: „Ni nani aliyeumba kinywa cha mtu? Ni nani amfanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi? Aone au awe kipofu? Je, si mimi Mwenyezi-Mungu? Basi nenda! Mimi nitakiongoza kinywa chako na kukufundisha cha kusema!“ (Kutoka 4: 11 +12)
5. Musa anajaribu tena: „Ee Bwana wangu, tafadhali nakusihi, umtume mtu mwingine.“ (Kutoka 4: 13)
- Mungu anamwambia Musa na hasira: „Je, si yuko ndugu yako Aroni ambaye ni Mlawi? Najua yeye ana ufasaha wa kuongea. …“ (Kutoka 4: 14) na mstari wa 16: „Aroni ataongea na Waisraeli kwa niaba yako. Yeye atakuwa msemaji wako, nawe utakuwa kama Mungu kwake.”
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
- Nani ameshawahi kuigizwa kwenda na kupeleka kitu au kumwabia mtu mwingine jambo fulani? Nani alikuigiza kitu gani au jambo gani?
- Ilikuwaje? Ulifanya au ulipata mashaka?
- Mashaka gani?
- Una changamoto gani ukipata changamoto kwa kazi zinazogizwa nawe na wazazi, ndugu, kaka, dada n.k.?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Leo tunajifunza kuhusu mtu mzima mmoja ambaye alijaribu mara tano kupingana na nini kilichomjibu kutoka Mungu. Tusikie kama Musa alimwambia Mungu mambo gani ili apingane na maigizo yake kutoka Mungu.
+Simulizi
„Miaka mingi alifanya kazi Midiani. Ameshaoa Sipora na alipata watoto. Ilikuwa siku moja… Kutoka 3: 11 – 22 na 4: 1 – 17 na 27 na 28
Maelezo ya maneno magumu ni ndani ya simulizi. Unasimulia maelezo na pia uonyeshe picha ya somo la leo.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Musa alikuwa akifanya kazi gani alipokaa jangwani?
- Jangwani ni sehemu ya namna gani?
- Alishangaa kwa kitu gani cha ajabu?
- Aliona kichaka kinawaka moto lakini ? Umalize sentenzi!
- Mungu alimwambia Musa kufanya nini?
- Musa ana mashaka mengi. Ana mashaka gani?
- Mungu alimwambia Musa nini kutoa mashaka yake?
- Mungu alitoa ishara gani kumsaidia Musa?
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Musa alikuwa akifanya kazi gani alipokaa jangwani?
- Jangwani ni sehemu ya namna gani?
- Alishangaa kwa kitu gani cha ajabu?
- Mungu alimwambia Musa kufanya nini?
- Musa ana mashaka mengi. Ana mashaka gani?
- Mungu alimwambia Musa nini kutoa mashaka yake?
- Mungu alitoa ishara gani kumsaidia Musa?
- Nani watamsaidia Musa kwenda mbele ya Farao na kuongea naye ?
Kazi ya mikono: Watoto watengeneze mfano wa kichaka kinawaka moto, lakini hakikuteketea katika mchanga au kuigiza habari hii, hasa mazungumzo katikati ya Mungu na Musa.
Wanaweza pia kuchora herufi za kiebrania kwa mchanga, daftari au ukurusa moja. Uangalie picha!
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Musa alikuwa akifanya kazi gani alipokaa jangwani?
- Ukiwachunga wanyama jangwani unapata changamoto gani?
- Alishangaa kwa kitu gani cha ajabu?
- Mungu alimwambia Musa kufanya nini kwa sababu alisikia maombi ya nani?
- Musa ana mashaka mengi hasa. Ana mashaka manne, yataje?
- Mungu alimwambia Musa nini kuondoa mashaka yake?
- Mungu alitoa ishara gani kumsaidia Musa?
- Nani watamsaidia kuongea na Farao?
- Musa alipomwua Mmisri aliyopenda kufanya kazi gani?
- Ni kazi ile ile lakini jambo gani sasa ni tofauti?
Kazi ya mikono: Watoto watengeneze mfano wa kichaka kinachowaka moto, lakini hakikuteketea katika mchanga au kuigiza habari hii, hasa mazungumzo kati ya Mungu na Musa.
Wanaweza pia kuchora herufi za kiebrania kwa mchanga, daftari au ukurusa moja. Uangalie picha!
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo unapatikana katika kitabu cha Kutoka 3: 12a na unasema: “… bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe!”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Nani anamwahidi nani hii?
- Mungu anamwahidi Musa nini?
- Jina lake la „MIMI NIKO AMBAYE NIKO“ lina maana gani kwa wewe?
- Mungu anapenda kukaa karibu pamoja nawe, jana, leo na kesho. Je, anamwahdi hili kwa Musa tu au kwa nani pia?
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kupita kuimba maneno haya.
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Kutoka 3. 12a na unasema: “… bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati:
- Nani anamwahidi nani hili?
- Mungu anamwahidi Musa nini?
- Jina lake la „MIMI NIKO AMBAYE NIKO“ lina maana gani kwako?
- Je, anamwahdi hili Musa tu au na akina nani pia?
- Ukiamini sentensi hii itakusaidia nini kwamba Mungu yupo pamoja nawe na atakuwa pamoja nawe?
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baada ya hii wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
Ziada: Mchezo: Kama una muda ufanye mchezo huu (chemsha bongo) na watoto wa umri wa kati na wakubwa!eUwachoree mchezo huu ubaoni. Uandike tu “Mimi niko ambaye niko” katikati kama unavyoona kwa mfano.
Maelezo mafupi: Watoto wakuambia maneno yanayohusiana na somo la leo kutoka Biblia. Na wewe uchaze visanduko mpaka vimeshajazwa na watoto. Herufi nyembamba zinazokusaida kujazkwa mchezo huu lakini ni pendekezo tu. Uandike herufi nene tu ubanoni! Maneno ya katikati: „Mimi niko ambaye niko!“
M | u | n | g | u | |||||||||
M | i | d | I | a | n | i | |||||||
M | o | t | o | ||||||||||
M | i | s | r | I | |||||||||
* | |||||||||||||
N | |||||||||||||
w | a | I | s | r | a | e | l | i | |||||
K | u | t | o | k | a | ||||||||
m | a | O | m | b | i | ||||||||
* | |||||||||||||
k | u | w | A | o | k | o | a | ||||||
M | u | s | a | ||||||||||
I | B | r | a | h | i | m | u | ||||||
H | A | r | u | n | i | ||||||||
Y | a | k | o | b | o | ||||||||
h | a | k | i | k | u | t | E | k | e | t | e | a | |
* | |||||||||||||
N | |||||||||||||
I | s | h | a | r | a | ||||||||
m | a | s | h | a | K | a | |||||||
p | a | m | O | j | a |
[/accordion-item]
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Kutoka 3: 12a na unasema: “… bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wakubwa:
- Nani anamwahidi nani hili?
- Mungu anamwahidi Musa nini?
- Jina lake la „MIMI NIKO AMBAYE NIKO“ lina maana gani kwa wewe?
- Je, anamwahdi hili Musa tu au na akina nani pia?
- Ukiamini sentensi hii itakusaidia nini kwamba Mungu yupo pamoja nawe na atakuwa pamoja nawe?
- Je, unaweza kutumia njia gani za kumtumikia Mungu katika maisha yako ya kila siku? Uongee kwanza na jirani yako! Halafu mtatuambia!
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Baadaye wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
Ziada: Mchezo: Kama una muda ufanye mchezo huu (chemsha bongo) na watoto wa umri wa kati na wakubwa!eUwachoree mchezo huu ubaoni. Uandike tu “Mimi niko ambaye niko” katikati kama unavyoona kwa mfano.
Maelezo mafupi: Watoto wakuambia maneno yanayohusiana na somo la leo kutoka Biblia. Na wewe uchaze visanduko mpaka vimeshajazwa na watoto. Herufi nyembamba zinazokusaida kujazkwa mchezo huu lakini ni pendekezo tu. Uandike herufi nene tu ubanoni! Maneno ya katikati: „Mimi niko ambaye niko!“
M | u | n | g | u | |||||||||
M | i | d | I | a | n | i | |||||||
M | o | t | o | ||||||||||
M | i | s | r | I | |||||||||
* | |||||||||||||
N | |||||||||||||
w | a | I | s | r | a | e | l | i | |||||
K | u | t | o | k | a | ||||||||
m | a | O | m | b | i | ||||||||
* | |||||||||||||
k | u | w | A | o | k | o | a | ||||||
M | u | s | a | ||||||||||
I | B | r | a | h | i | m | u | ||||||
H | A | r | u | n | i | ||||||||
Y | a | k | o | b | o | ||||||||
h | a | k | i | k | u | t | E | k | e | t | e | a | |
* | |||||||||||||
N | |||||||||||||
I | s | h | a | r | a | ||||||||
m | a | s | h | a | K | a | |||||||
p | a | m | O | j | a |
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na masomo haya. Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto watafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisi kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).