+Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watajifunza ya kuwa dhambi haiwezi kufichwa.
- Watagundua kwamba Mungu mwenyewe amemwandaa Musa mpaka yeye ni tayari kutumika kwa Mungu na kuheshima maisha na uhai wa watu wengine.
- Watakuwa tayari kutubu makossa yao na kumfuata Mungu kwa njia ya kutumia utendaji mzuri na watu wengine.
+Maelezo juu ya somo
Tunajua Musa ni mtoto wa mama ya kiebrania. Lakini aliipata bahati na alilelewa katika mila na desturi na hasa hekima za Misri kama mtoto wa kifalme kwa sababu binti ya Faroa alimchagua alipokuwa na miaka michache ya kipindi cha utoto. Kwa hiyo alisomo shuleni kama mtoto mwingine wa Farao. Alijifunza hekima yote iliyotakiwa katika Misri. Pia tunaweza kusema alizoea kuyaongoza majeshi ya Farao na kufahamu mpango wa vita.
Walakini alijua asili yake na kufahamu ya kuwa Waisraeli walioteswa vikali katika utumwa wao walikuwa ndugu zake. Hii pia Musa hakuweza kujificha na yeye mwenyewe alikwenda kuwatembelea ndugu zake na kuongea nao.
Pia tunasoma ndani ya ufafanuzi wa Biblia kwamba Musa alikuwa na umri wa miaka arobani alipomwua mtu mwingine na kukimbiliia Midiani. Musa alifikiri yeye mwenyewe kwa uwezo wake na nia yake njema (kumwua Mmisri) anaweza kuwakomboa Waebrania/Waisraeli wenzake , kutoka kipindi kigumu cha utumwa. Lakini alikosa sana ndani ya wazo lake. Ni Mungu mwenyewe anayeweza kuwakomboa wao na sisi. Musa alijiamini sana kwamba aliweza kuwasaidia Waebrania/Waisraeli mpaka aligundua wenzake hawakufurahi kwamba yeye anapenda kuonekana kama kiongozi wao.
Kwa hiyo ilitakiwa Musa ajifunze kutokujiamini mwenyewe, na pia alipaswa kujifunza kusubiri wakati wa Mungu. Ilikuwa ni Mungu, sio Musa, ambaye angeliwakomboa Waebrania.
Alipokimbia Midiani alianza kujifunza mambo mapya kabisa. Mungu alimpa mafundisho mapya kuhusu utendaji mbaya wa binti za Yethro kisiwani. Musa alimwoa Sipora. Musa alikaa miaka 40 tena Midaini.
Kwa ujumla tunaweza kusema palikuwa na mambo matatu hasa ambayo yaliongoza mwelekeo wake mpya. Mambo haya yalikuwa mateso ya Waebrania, mapigano kati ya wanaume wawili wa Kiisreali na utendaji mbaya wa binti za Yethro. Alihitaji muda mrefu kujifunza mpaka yeye ni tayari kumwelewa Mungu.
Kwa hiyo tunaweza kusema kumfuata Mungu na kumwelewa Mungu kwa maisha yetu muda unatumika sana mpaka miaka mingi maishani mwetu.
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
Maelezo mafupi: Kipindi cha utumwa chini ya Farao wa Misri watumwa walijenga mafotali katika majengo ya serikali kwa upana ya meta moja. Na kama wakilazimishwa kujenga ukuta kwa ajili ya kuzuia mjini walijenga ukuta menye upana wa meta 15 mpaka 18. Pia kuta zilijengwa kwa urefu sana. Kwa hiyo Farao na wanayapala walihitaji matofali mengi sana. Walitumia watumwa kufanya kazi hii. Na leo tunaigiza kama sisi wote ni watumwa kwa kipindi hiki. Ninakueleza kwanza halafu tutafanya pamoja:
Watoto wote waigize vitendo fulani. Ufuate picha zinazoeleza vitendo vya watumwa kipindi cha Farao na Musa
Uangalie picha ya 1 mpaka 8
- Watumwa wanachota maji => watoto wanaiga kama wanachota maji.
- Watumwa wanachanganya mchanga na “cementi” => watoto wanaiga kuchanganya mchanga na “zementi”.
- Watumwa wanabeba ndoo zenye mchanga => watoto wanabeba ndoo (bila mchanga); wanaiga tu.
- Watumwa wanafyatua matofali na wanainama. => watoto wanaiga kitendo hicho.
- Watumwa wanapanga matofali => watoto wanaiga kama wanapanga matofali.
- Watumwa wabeba matofali kwa kutumia msega => watoto wanafanya hivyo na wajue ni mzito sana.
- Watumwa wanajenga majengo makubwa chini ya Farao na wanyapala (viongzi wa kazi; wanyapala wamewapiga watumwa kwa fimbo ya ngozi kuwaharakisha wao kwa kazi zao => watoto wanaiga kama wanajenga majengo na mmojawapo ni mnyapala (kiongozi)wao; anaiga tu kama anawapiga na fimbo yenye ngozi.
- Watumwa wanakaa chini ya wanyapala wakali => watoto wanaiga ukali wa wanyapala. “Usichoke!” – “Usimame, ufanye kazi kwa haraka!” – “Wewe ni mvivu – uendelee na kazi yako! Hatukulipi kwa kupumzika!” n.k.
- Watoto wote wafanye hii. Kama wakielewa mfumo huu ni lazima kufanya kwa haraka zaidi. Viongozi wao “wanawapiga” kwa fimbo yenye ngozi kama hawajafanya kazi ndani ya muda au watumwa wakionyesha upungufu au uchovu.
- Baada ya mchezo huu uongeze muda mfupi na watato. Ukifanya kazi hii kama wao watumwa:
- “Je, huwezi kukasirika ukifanya kazi kama wao? Ukifanya kazi kama watumwa unakasirika kwa kitu gani ndani ya kazi za utumwa?”
- Ukikasirika itakuwaje? Unafanya nini?
- Ukikasirika inaleta changamoto na hasara gani?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Leo tunajifunza kuhusu mtu mmoja ambaye alikasirika kutoka Agano Kale na hasira yake ilileta mwelekeo gani ndani ya maisha yake. Tusikie nini ilitokea naye baada ya hasira yake.
+Simulizi
„Miaka mingi, kama 40, iliyopita na Musa sasa ni mtu mzima. … Kutoka 2: 11 – 22 au mpaka 25 katika rika zote.
Maelezo ya maneno magumu ni ndani ya simulizi. Unasimulia maelezo na pia uonyeshe picha ya somo la leo.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Musa alijifunza nini kaitka utoto wake?
- Kwa nini alikasirika na kumwua yule Mmisri?
- Kwa nini alitoroka Midiani?
- Alifanya nini Midiani?
- Alikaa muda gani Midiani?
Maelezo mafupi: Musa alifikiri yeye ni mkubwa kuliko wengine na anaweza kuwakomboa wenzake ambao wanaishi katika mateso makubwa. Lakini Mungu alipanga mpango mwingine naye. Kwa hiyo Musa aliendelea kujifunza mambo ya Mungu na maisha yake.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Musa alijifunza nini katika utoto wake? Kwa sababu gani?
- Alikasirika na alifanya kitu kibaya sana. Alifanya nini kwa Mmisri?
- Alifikiri nini alivyomwua Mmsiri na kumficha mchangani?
- Kwa nini alitoroka Midiani?
- Alipofika Midiani, sehemu ya jangwa nini kilichotokea? Alimsaidia nani?
- Musa alifanya nini Midiani kwa muda gani?
Maelezo mafupi: Musa alipata mafundisho kama kila mtoto wa mfalme na Farao. Alijua kusoma na kuandika na mambo mengi ya desturi na heshima mambo ya kimisri. Alizoea sana maisha makubwa kuliko wenzake. Lakini alijiamini sana na alifikiri anaweza kuwakomboa wenzake Waebrania. Mungu alimsaidia kujifunza mambo ya imani, kwamba Mungu tu anayeweza kuwakomboa kwa muda wake Waebrania. Kwa hiyo Musa alijifunza ndani ya miaka 40 tena mambo ya imani na Mungu sehemu ya ugenini kwake. Alipotoroka alikuwa umri wa miaka 40 pia.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Musa aliishije? Alijifunza mambo gani alipokua katika kipindi cha utoto na ujana wake?
- Alikasirika kwa sababu gani? Alifanya nini ndani ya hasira yake?
- Kwa nini hajafaulu kuyafisha makosa yake?
- Kwa nini alitoroka Midiani?
- Nini ilitokea Midiani alipofika? Aliwasaidia nani na kwa sababu gani?
- Alipokaa miaka 40 katika Midiani alifanya kazi gani?
- Mungu alimpa mafundisho gani na kwa sababu gani kule Midiani?
Maelezo mafupi: Musa aliishi miaka 40 kama mfalme na halafu aliishi miaka 40 jangwani maisha tofauti. Bado hajajifunza vizuri kumwelewa Mungu na kumfuata Mungu vizuri. Alihitaji kupitia makosa kama kumwua mtu, kujiamini kupita kiasi, kufikiri anaweza kuwakomboa wenzake. Mungu alimpeleka mpaka jangwani ili Musa ajifunze kumtegemea Mungu na kumfuata ina maana gani. Kama tukijua tulifanya makosa gani ndani ya maisha yetu, tunaweza kutubu mbele za Mungu, kubadilika na kuanza maisha mapya kama Musa. Lakini ni mafundisho ya maisha na imani.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Hesabu 32: 23a na unasema: “Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za Bwana.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Mungu ametupa amri fulani kwa ajili ya kuyatunza maisha ya watu wengine. Kama hupendi kufuata amri zake unafanya nini mbele ya Mungu?”
- Unaweza kufanya dhambi gani kwa umri wako?
- Ukikosa na ukifanya dhambi mara nyingi watu wanagundua. Wakigundua umekosa na umefanya dhambi wajisikiaje?
Maelzo mafupi: Mungu hafurahi kwa dhambi zetu na makosa yetu lakini bado anatupenda. Upendo wake ni mkubwa. Kwa hiyo tujaribu kumtafuta Mungu kwa matendo mazuri kwa ajili ya kumfurahisha na kurudhisha upendo wetu naye kwa njia hii.
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kama kawaida.
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka Hesabu 32: 23b na unasema: ”…, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata hapana buni.“
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati:
- Watoto kwa umri wako wanaweza kufanya dhambi gani?
- Ukiangalia amri za Mungu. Kwa nini alitupa amri hizi?
- Tukifanya dhambi nini kinatokea?
- Tukifanya dhambi matokea gani yanakuja kwa uhusiano wa Mungu na watu wengine?
Maelezo mafupi: Mungu akiona dhambi zangu anajua sisi tumekosea. Lakini pia ana upendo mkubwa na amemleta Yesu, mtoto wake, kwa ajili ya kuharibu ubaya wetu kutokana na dhambi zetu na yeye, Mungu mwenyewe. Alijenga tena kwa ajili ya kifo cha Yesu uhusiano mwema kati ya yeye Mungu na sisi. Swali letu ni „Je, wewe ni tayari kupunguza dhambi na matendo mabaya, ili uweze kujisikia upendo wa Mungu zaidi? Je, wewe ni tayari kuonyesha utendaji mzuri na upendo wako kwa watu wengine, kama Yesu alitufundisha kuonyesha upendo wa Mungu?“ Ufikiri kwa maswali haya kidogo.
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka Hesabu 32: 23 na unasema: “Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za Bwana, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata hapana budi.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wakubwa:
- Kwa umri wako watoto wanafanya dhambi gani?
- Kama watoto au binadamu akifanya dhambi anajitoa kutoka upendo wa Mungu? Inaleta kitu gani kwa maisha yake akikaa mbali na Mungu?
- Dhambi na utendaji mbaya uanaleta nini?
- Tukifanya vibaya kwa ndugu, marafiki na jirani inaleta uhusiano namna gani na wao?
Maelezo mafupi: Tukifanya dhambi maana ni tunaenda mbali na Mungu. Hatukai tena karibu naye. Kama hatukai tena karibu naye tutapata hasara katika maisha yetu. Mungu anajua hii kwa hiyo ana upendo mkubwa. Anapenda kutusaidia mara nyingi. Lakini jambo muhimu sisi kuwa ni tayari kubadilisha utendaji wetu. Je, weweupo tayari? Ufikiri kidogo kuhusu swali!
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Baadaye wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na masomo haya. Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto watafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisi kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).