+Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watafahamu jinsi Mungu anavyowalinda watu wake na kuwawezesha ili wafanye kazi kwa neema yake.
- Watatambua kwamba Waisraeli walipata mateso makubwa chini ya Farao lakini Mungu ana mpango malumu na taifa lake.
- Watakuwa waangalifu kusubiri kuelewa mpango wa Mungu kwa kila mtoto ingawa tutaweza kuona baadaye sana na anapenda kumlinda kila mtoto kutoka siku ya kuzaliwa kama alivyomlinda mtoto wake Musa.
+Maelezo juu ya somo
Tunaingia sasa kipindi kigumu sana kwa Waisraeli. Pia tunaangalia nyuma kabisa kutoka leo kwa wakati wa mwanzoni mwa historia ya Waisraeli.
Waisraeli waliishi kama miaka minne katika Misrini kwa hiyo ni rahisi kumsahau Yusufu na familia yake na nini alifanya kwa Misri kipindi cha nyuma. Familia ya Yusufu na wengine wa mataifa mengine, wote waliongezeka kwa haraka na hasa ndugu kutoka familia ya Yusufu walioanza kuwa taifa kubwa ndani ya nchi ya Misri. Farao mpya alikuwa tofauti na Farao wa zamani aliyemkaribisha Yusufu katika ufalme wake na kumtumia Yusufu kama msaidizi wake.
Farao mypa hakufurahi na taifa kubwa la wana wa Israeli. Mtazamo wake wa Farao mpya ulikuwa tofauti kabisa. Aliwaogapa sana Wairaeli kwamba watafanya ubaguzi ndani ya nchi yake kwa hiyo alijaribu kutumia njia mbalimbali kuwapungua:
Kwanza Farao mpya alikuwa amewafanya Waisraeli kuwa watumwa. Ni mifano mitatu inaeleza mambo haya:
1) waliwekwa kwenye kazi za kulazimishwa (1: 8- 14),
2) wakunga wao waliamriwa waue watoto wote wa kiume wakati wa kuzaliwa (1:15 – 21) na
3) walipokataa kuwa na ushirikiano, amri zilizotolewa za kuwatupa kwenye mto Naili watoto wote wa kiume wa Kiisraeli waliozaliwa (1: 22) Hii ilikuwa kazi ya maaskari sio wakunga tena.
Lakini pia wakunga walilazimika kuchagua kati ya kumtii Mungu na kumtii Farao (maana kwa kimisri kama “mtoto wa mungu au mungu mwenyewe” pia). Wakungu walitoa uamuzi kumtii Mungu sio Farao. Na walifanya uamuzi huu kwa kuhatarisha maisha yao.
Ukiangalia matukio yanayoeleza kuzaliwa kwa Musa unaweza kugundua kwama maandiko yanaonyesha wazi ufanyaji kazi wenye nguvu na majaliwa ya Mungu. Mungu alitumia mazingira, watu mpaka binti Farao na vitu vya kuasili kumlinda Musa na kulinda uhai wake.
Tukimwangalia binti Farao tunaweza kugundua mambo machache wakuu pia. Yeye anajua huyu mtoto ni mtoto wa mama la kiebrania na pia jina lake ni kiebrania (Musa =kutolewa kwenye maji). Lakini jina la Musa lina maana nyingine pia “aliyezaliwa na” kama Thutmose na Ahmose. Maana ni huyu aliyezaliwa ndani ya familia na Thut au Ah maana ni mwana wa Thut au Ah.
Tunaweza kuona kuna kiasi cha kejeli katika ukweli kwamba binti Farao ambaye ni binti wa mkandamizaji mwenyewe anamwinua yule ambaye atakomboa watu wanaodhalilishwa na kudhoofishwa na huyu Farao (mkandamizaji).
Kama mtoto wa kiume wa binti wa Farao, Musa aliingia na aliishi kwenye familia ya kifalme. Musa mwenyewe kama jina lake linaeleza ni mtu wa waibrania na mtoto wa mfalme. Ni mtu ambaye anajua lugha ya Kiebrania na Kimisri vizuri sana. Pia ni mtu ambaye anazoea kuwa na nguvu kama mfalme na mtu mkubwa lakini pia kuona huruma kwa wenzake.
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
- Nani ameshawahi kupata mdogo wake?
- Huyu mtoto mchanga alikuwaje?
- Mtoto mchanga anafanya nini?
- Mama na baba yake wanachangamoto gani na huyu mtoto mchanga?Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Leo tunajifunza kuhusu mtoto mchanga mmoja na kitu gani kilichotokea kwake kwa maisha yake.
+Simulizi
„Ilikuwa muda mrefu nyuma kutoka leo…“ Kutoka 1: 8 – 14, 22; na 2: 1 – 10 katika rika zote
Ueleze muda mfupi na kwa sentisi chache mistari ya Kutoka 1: 8 – 14 na 22 na uweke umakini kwa somo la Kutoka 2: 1 – 10 zaidi. Maelezo ya maneno magumu uweke ndani ya simulizi. Usimulie maelezo! Uonyeshe picha ya somo la leo!
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Musa alizaliwa katika familia gani?
- Mama alipata huzuni na alihangaika sana. Kwa nini?
- Mama yake na Mariamu, dada mkubwa walifanya nini?
- Mariamu alipata wazo gani kumsaidia binti wa Farao?
- Binti wa Farao alimpa jina gani? Jina lake lina maana gani?
Maigizo: Watoto wanaweza kuigiza somo hili. Au wanaweza kuchora picha kuhusu somo hili ndani ya dafari lao au wanaweza kujenga mfano wa safina katika mchanga.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Familia ya Musa walipata shida gani kipindi cha Farao wakati Musa alipozaliwa?
- Baada ya muda gani mama yaka alifanya nini? Kwa sababu gani?
- Ni nani aliyemwona Musa kando la mto?
- Miriamu alimleta nani kumtunza mtoto? Alipata wazo gani kumsaidia binti wa Farao?
- Binti wa Farao alimpa jina gani na lina maana gani?
- Musa ana kama familia mbili, kwa nini? Amelelewa kwa familia mbili, kwa sababu gani?
Maigizo: Watoto wanaweza kuigiza somo hili. Au wanaweza kuchora picha kuhusu somo hili ndani ya dafari lao au wanaweza kujenga mfano wa safina katika mchanga.
Labda mchezo wa “Kuwaficha watoto”: Pia watoto wanaweza kucheza mchezo “Kuwaficha watoto”maana ya kuvificha vitu. Mwalimu analeta midoli kutoka mahindi, picha za watoto au mawe madogo (kokoto). Labda mawe yanafunguliwa na kubaki na vitenge. Halafu nusu ya idadhi ya watoto wanaruhusiwa kuvificha vitu hivi. Picha moja, mdoli mmoja au jiwe moja (yenye kitenge)ni Musa.
Kama nusu ya idadi ya watakapokuwa wakificha vitu wengine wanaweza kuvitafuta vitu hivyo. Lakina wanapewa muda kama dakika tano. Kwa kili kitu (kama picha, mdoli au jiwe kikundi cha pili wanapata alama kutoka “Farao” ambaye ni mwalimu mmojawapo. Wakipata picha, mdoli au jiwe la kikundi cha pili wanapewa alama 5. Kama wao wanaopata “mtoto Musa” maana kama picha ya Musa, mdoli wa Musa au jiwe la Musa, wanapata alama 10.
Pia kikundi cha kwanza wanapata alama 5 kutoka “Farao” kwa kila kitu (picha, mdoli au jiwe)ambalo kilichofichwa na watoto hawajakiona. Kwa “Musa” ni alama 10.
Mwishoni kwa mchezo huu “Farao” anafanya mahesabu ya alama zote za kikundi cha kwanza na cha pili. Halafua atatangaza kikundi gani wameshinda.
Kama una muda kikundi cha pili sasa wanaweza kuvificha vitu na kikundi cha kwanza watavifuta.
Pia kwa mwisho kabisa ya sehemu hii uongee na watoto kuhusu Mungu anaweza kuwalinda watoto katika maisha yao. Pia tutie moyo kwamba Mungu ana mpango kwa kila mtu na mtoto wake, lakini hatuwezi kuona leo mpango wake. Kama Mungu alikuwa na mpango na Musa na hili tutajifunza Jumapili ijayo.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Kipindi kilikuwa kigumu cha kuzaliwa kwa Musa. Kwa nini?
- Kwa nini mama wa Musa alimficha nyumbani na baadaye ndani ya kisafina?
- Binti wa Farao alipenda kufanya nini na mtoto mchanga?
- Dada mkubwa wa Musa, labda Mariamu, alifanya nini alipomwona binti wa Farao? Miriamu alimleta nani kumtunza mtoto?
- Binti wa Farao alimpa jina gani na lina maana mbili ni zipi?
Maigizo: Watoto wanaweza kuigiza somo hili. Au wanaweza kuchora picha kuhusu somo hili ndani ya dafari lao au wanaweza kujenga mfano wa kisafina cha Magugu au mbao.
Labda mchezo wa “Kuwaficha watoto”: Pia watoto wanaweza kucheza mchezo wa “Kuwaficha watoto”maana ya kuvificha vitu. Mwalimu analeta midoli kutoka mahindi, picha za watoto au mawe madogo (kokoto). Labda mawe yanafunguliwa na vitenge. Halafu nusu ya idadi ya watoto wanaruhusiwa kuvificha vitu hivyo. Picha moja, mdoli mmoja au jiwe moja (yenye kitenge)ni Musa.
Kama nusu ya idadi ya watakapokuwa wanavificha vitu wengine wanaweza kuvitafuta vitu hivi. Lakina wanapewa muda kama dakika tano. Kwa kili kitu (kama picha, mdoli au jiwe kikundi cha pili wanapata alama kutoka “Farao” ambaye ni mwalimu mmojawapo. Wakipata picha, mdoli au jiwe la kikundi cha pili wanapewa alama 5. Kama wao wanaopata “mtoto Musa” maana kama picha ya Musa, mdoli wa Musa au jiwe la Musa, wanapata alama 10.
Pia kikundi cha kwanza wanapata alama 5 kutoka “Farao” kwa kila kitu (picha, mdoli au jiwe)ambacho kilichopotea na watoto hawajakiona. Kwa “Musa” ni alama 10.
Mwishoni kwa mchezo huu “Farao” anafanya mahesabu ya alama zote za kikundi cha kwanza na cha pili. Halafu atatangaza kikundi gani wameshinda.
Kama una muda kikundi cha pili sasa wanaweza kuvificha vitu na kikundi cha kwanza watavitafuta.
Mwishoni kabisa wa sehemu hii uongee na watoto kuhusu Mungu anaweza kuwalinda watoto katika maisha yao. Pia kuwatia moyo kwamba Mungu ana mpango kwa kila na mtu na mtoto wake, lakini hatuwezi kuona leo mpango wake. Kama Mungu alikuwa na mpango na Musa na hii tutajifunza Jumapili ijayo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Yeremia 1:5 na unasema: “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;…”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Nani anakufahamu tangu ulipokaa tumboni mwa mama?
- Nani amekuumba?
- Mungu anakufurahia wewe kwa sababu gani?
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kupita isahara inayoelezwa:
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Yeremia 1:8 na unasema: „Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asama Bwana”
Maswahli kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati:
- Bwana ni nani?
- Na anapenda usipate nini?
- Mungu anapenda kukufanyie nini?
- Mungu anapenda kukulinda kama Musa. Anapenda kukaa karibu nawe kama Musa. Uliona msaada wapi ndani ya maisha yako?
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Zaburi 50:15 na unasema: „Ukanitii siku ya mateso, nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”
Maswahli kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa kubwa:
- Mungu anatoa ahadi gani?
- Anapenda unamfanyie nini?
- Mateso gani watoto wa umri wako wanaweza kupata?
- Anapenda kukaa karibu nawe na kukulinda. Kwa sababu gani?
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo. Halafu wachore picha ya mstari wa moyo inayoonyeshwa na watoto wakubwa chini ya maandiko yao. Wakitumia ukurasa mdogo wachore picha nyuma ya ukurusa huu! Pia waandike mifano miwili Mungu aliwasaidia kwa mambo magumu (= mateso) gani ndani ya maisha yao.
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na masomo haya kuhusu „Tutoe kwa moyo.“ Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto watafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisi kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).