+Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watajifunza kuwa watu wote ni jirani zetu kwa hiyo inatupasa kuwapenda.
- Watagundua kwamba mtu ambaye anatuhitaji ni jirani yetu kama ni jirani kweli au jirani ghafla kwa sababu anatuhitaji.
- Watafurahi kuwasaidia wengine ndani ya maisha yao na watakuwa jirani wema katika mazingira yao.
+Maelezo juu ya somo
Mwalimu aangalie ramani ya Nchi Takatifu wakati wa Kristo katika Biblia yake. Jimbo la Samaria ni katikati ya Galilaya na Uyahudi. Wenyeji wa Samaria walidharauliwa na kuambiwa walikuwa chotara na waliopotea katika dini. Tangu wakati wa Nehemia na Ezra uadui ulikuwa kati ya Wayahudi na Wasamaria na katika siku za Kristo hawakuchangamana hata kidogo.
Kuhani na Mlawi walikuwa watu walioheshimiwa katika nchi ile.
Mwalimu na wanafunzi watengeneze mifano ya milima mirefu yenye njia nyembamba na nyumba ya wageni. Watumie vijiti kuwa mifano ya watu wakati wa kusimulia habari hii. (Uangalie kielelezo!)
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
- Nani ameshawahi kusaidiwa?
- Wamekusaidia kwa jambo gani?
- Wewe umewasaidia watu wengine kwa tendo gani?
- Ukiwasaidia wengine inaleta faida gani?
Kujenga „daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Leo tunajifunza kuhusu mfano mmoja kutoka kwa Yesu na faida gani kwa mtu ambaye alipata shida kubwa na amesaidiwa na mgeni. Lakini pia tunasikia kuhusu mwana-sheria aliyependa kujua anahitaji kufanya nini ili aishi milile.
+Simulizi
Maelezo ya maneno magumu ni ndani ya simulizi. Usimulie maelezo! (k.m. Mwana-sheria)
Uonyeshe picha ya somo la leo!
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Yesu alionana na mwana sheria na ndani ya mazungumzo haya alimweleza mfano mmoja wa msafiri. Je, nini kimetokea kwa huyu msafiri?
- Mtu wa kwanza huyu kuhani alimsaidia huyu ambaye alipigwa na majambazi? Kwa sababu gani?
- Mtu wa pili, huyu Mlawi, alimsaidia? Ana sababu gani kutomsaidia?
- Mtu wa tatu alimsaidi huyu ambaye alipigwa na majambazi? Ana sababu gani?
- Kwa hiyo Yesu alimshauri mwana sheria nini mwishoni mwa mazumgumzo yao?
Maelezo mafupi: Tukimpenda Mungu wetu kwa moyo wetu wote au ukimpenda Mungu wako kwa moyo wako wote utakuwa tayari kumsaidia mtu mwingine pia, kama ni ndugu, rafiki, jirani au mtu mwingine.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Mwana-sheria ni nini? Ni mtu wa namna gani? Anafanya nini?
- Mwana-sheria alipenda kujua nini kutoka kwa Yesu? Alimwuliza nini?
- Yesu alimjibu na mfano moja wa msafiri. Unieleze mfano huu!
- Kuhani na Mlawi walifanya nini walipomwona huyu mtu ambaye alipigwa na majambazi?
- Msamaria alifanya nini na kwa sababu gani?
- Mwishoni Yesu alimwuliza mwana-sheria nini? Yesu alimwambia nini huyu mwana-sheria?
- Kwa hiyo unafikiri sisi tunaweza kufanya nini kuonyesha kwamba sisi tunampenda Mungu?
Maelezo mafupi: Tunaweza kusema: Tukimpenda Mungu kwa moyo wote tunaweza pia kumsaidia mtu mwengine kama ndugu, rafiki, jirani au mgeni. Kwa sababu tunaona Mungu anavyotupenda na sisi tunampenda Mungu kwa hiyo tupo tayari kumsaidia mtu ambaye anahitaji msaada wetu.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Mwana-sheria ni nini? Ni mtu wa namna gani? Anafanya nini?
- Mwana-sheria alipenda kujua nini kutoka kwa Yesu? Alimwuliza nini?
- Yesu alimjibu akitumia mfano mmoja wa msafiri. Unieleze mfano huu!
- Kuhani na Mlawi walifanya nini walipomwona huyo mtu ambaye alipigwa namajambazi?
- Msamaria alifanya nini na kwa sababu gani?
- Mwishoni Yesu alimwuliza mwana-sheria nini? Yesu alimwambia nini huyu mwana-sheria?
- Kwa hiyo unafikiri sisi tunaweza kufanya nini kuonyesha kwamba sisi tunampenda Mungu?
Maelezo mafupi: Tunaweza kusema: Tukimpenda Mungu kwa moyo wote tunaweza pia kumsaidia mtu mwingine kama ndugu, rafiki, jirani au mgeni. Kwa sababu tunaona Mungu anavyotupenda na sisi tunampenda Mungu kwa hiyo tupo tayari kumsaidia mtu ambaye anahitaji msaada wetu.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Luka 10: 27a na unasema: “Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote…!”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Mungu anapenda kuona unampenda nani?
- Umpenda Mungu kwa moyo wako maana uanafanya nini?
Maelezo mafupi: Tunaweza kuongea naye kwa sala, tunaweza kwenda kanisani katika ibada ya watoto /Shule ya Jumapili, tunaweza kujifunza Neno lake. Pia tunaweza kuwasaidia wengine n.k..
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kupita isahara zinazoelezwa.
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Luka 10: 27a na unasema: “Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako!”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati:
- Mungu anapenda tumfanyie nini?
- Kwa nini anasema tumpende kwa moyo, roho, nguvu na akili?
- Pia anapenda tuwapende nani?
- Na nani mwingine?
Maelezo mafupi: Kama tukimpenda Mungu kama tunavyompenda jirani na kama nafsi zetu ni rahisi kumpenda mtu mwingine kama ndugu, rafiki, jirani na mgeni. Na kama tukijua Mungu anatupenda na sisi tunampenda Mungu tunaweza kusaidiana kama tukikaa ndani ya changamoto.
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Luka 10: 27a na unasema: “Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako!”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wakubwa:
- Mungu anapenda tumfanyie nini?
- Kwa nini anasema tumpende kwa moyo, roho, nguvu na akili?
- Pia anapenda tuwapende nani?
- Na nani mwingine?
Maelezo mafupi: Kama tukimpenda Mungu kama tunavyompenda jirani na kama nafsi zetu ni rahisi kumpenda mtu mwingine kama ndugu, rafiki, jirani na mgeni. Na kama tukijua Mungu anatupenda na sisi tunampenda Mungu tunaweza kusaidiana kama tukikaa ndani ya changamoto.
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Baadaye wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au katika nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
Kama una muda ufanye mchezo huu wa (chemsha bongo) na watoto wa umri wa kati na wakubwa!U wachore mchezo huu ubaoni.
Ziada: Mchezo:
Maelezo mafupi:
Tunaweza kusema, tukimpenda Mungu kwa moyo wote tunasaidia pia mtu mwingine kama ni ndugu, jirani au mgeni.
N | B | W | Y | U | P | E | N | D | O | S |
A | I | R | E | H | S | A | N | A | W | M |
F | R | S | S | K | H | B | Z | T | Q | U |
S | Q | P | U | I | U | T | W | I | S | N |
I | U | A | W | R | G | H | M | A | T | G |
Z | L | K | L | Z | F | K | A | K | N | U |
M | S | A | M | A | R | I | A | N | W | A |
I | N | A | R | I | J | P | B | G | I | Z |
Maneno 10 yanoyofatilia ndani ya mchezo wa chemsha bongo!
Yesu – Mwanasheria- Kuhani – Mlawi – Msamaria – Mungu – Upendo – Jirani – Nafsi – Bwana
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na somo hili kuhusu sala na maombi . Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto wanafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).