+Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watasikia kwamba wanawake wawili wametoa vitu vyao kwa moyo na kumpa Mungu ama Yesu.
- Watatamani kutoa vitu vyao pia kwa moyo na kumpa Mungu kwa sababu tunampenda.
- Watakuwa waangalifu kufanya hili kwa upendo wa moyo wao badala ya kutoa fedha nakupata sifa kutokea kwa watu wenigne.
+Maelezo juu ya somo
Kuhusu somo la Marko 12: 41 – 44: Sadaka ndogo kwa mama mjane/Utoaji wa KweliKwa hiyo ilikuwa rahisi kujua, kila mmoja aliweka shilingi ngapi ndani ya sanduku.Katika habari hii Yesu hakusema kuwa matajiri hawakutoa sadaka, lakini alisema kuwa yule mjane aliyempa Mungu yote aliyokuwa nayo alikuwa mkarimu sana. Alitoa kwa moyo kwa sababu alimpenda sana Mungu. Wanaoongoza hekalu walitumia njia hii kupata fedha kwa hiyo walifurahi zaidi kupata fedha nyingi kutoka kwa matajiri. Walimu wa sheria waliwakilisha wale waliokuwa wachoyo na wakitumia dini mara nyingi kama kisingizo.
Lakini pia kutoka maoni ya Yesu/Mungu huyu mjane alitoa nyingi ingawa ni cent mbili tu, laikini alitoa fedha zote. Kwa centi mbili angeweza kulipa chakula kimoja kwa siku ile. Lakini alitoa kutoka mioyoni mwake na alitoa kila kitu.
Wengine kama matajiri fulani walitoa fedha nyingi, ingawa wana fedha zaidi na hii ni kiasi kidogo tu kutoka mali yao. Walipenda kusifiwa. Walijua huyu ambaye alisimama karibu na sanduka atakuwa alikitangaza kiasi chao walichotoa.
Pia wajane kwa kipindi kile walikuwa maskini. Hakuna mtu aliwasaidia kuishi vizuri. Lakini pia walivaa nguo kutoka ngozi ya Mbuzi wa rangi nyeusi. Walionekana kwa urahisi wa mkiwabali kabisa kwa sababu mavazi yao.
Sanduku la hazina lilisimamishwa katika ua wa wanawake la hekalu, mahali palipoonekana. Na waliweka masanduku 13 ya hazina. Kwa hiyo Yesu mwenyewe alikaa karibu na sanduku moja. Kwa kawaida hutangaza kiasi cha fedha na watu kilichowekwa na watu ndani ya sanduku. Ratiba ilikuwa kama hii: Huyu alitoa alisema ni kiasi gani na huyu ambaye alisemama karibu na sanduku alifanya mahesabu na halalfu kiasi kilitangazwa kwa sauti
Yohana 12: 1 – 8 Yesu apakwa marashi na Mariamu Dinari moja ilikuwa mshahara wa kutwa kwa mfanyakazi siku zile. Na yeye amelipa dinari 300 maana amelipa kiasi cha mshahara wake kwa karibu mwaka mzima kwa marashi tu.Mariamu wa Bethania alifanya bila kufikiri zaidi. Alinawisha/alimwosha miguu ya Yesu kumwonyesha anavyompenda na aliipanguza miguu yake kwa nywele zake. Wanawake kwa kipindi kile hawaruhusiwi kutoka nyumba bila kuzifunga nywele zao. Utamaduni hakuwa ruhusa kuacha nywele wazi nje ya nyumba. Ni lazima wazifunge nywele zao.
Mariamu alimpaka Yesu marharmu ya nardo. Kawaida mfalme hupakwa na marhamu au siku ya mazishi ya mtu. Kwa hiyo tunaweza kusema alimpaka marhamu mfalme lakini pia kwa mtu ambaye atakufa karibuni. Na Yesu alijua hivi. Alifika nyumbani kwa Lazaro na Mariamu siku sita kabla ya sherehe ya Pasaka. Pia nyumba ya Lazaro ilijendwa katika kijijini ambacho ni kilomita 3 au maili 2 kutoka Yerusalemu. Kwa hiyo alikuwa katika ukanda wa hatari wa Yesu.
Kwa utamaduni wa Wayahudi na kipindi cha Agano Jipya ulikuwa mtu mwenye nyumba amwambie mtumwa kunawisha miguu ya wageni. Lakini yeye alisahau kufanya kama hivyo.
Mariamu wa Bethania ni mwanamke mwingine aliyetoa katika moyo na mchango wake alikuwa wa pekee sana kwa kutoa. Alikuwa na kibweta cha marhamu ya nardo safi yenye thamani kubwa. Alitaka kuonyesha wazi jinsi alivyompenda Bwana. Wanafunzi hawakujali upendo wake bali walitaka kumkemea kwa kupoteza ile marhamu.
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
- Nani ameshapata fedha kutoka kwa wazazi au ndugu wengine?
- Ukipata fedha kama elfu mbili, elfu tano au labda eflu kumi unaweza kufanya nini na fedha hizo?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Tunaweza kutumia fedha kwa njia mbalimbali na leo tunasikia kutoka wanawake wawili walifanya nini na fedha zao. Pia tunajifunza kutoka kwa Yesu alisema nini kuhusu wanawake wawili kwa matumizi ya fedha zao.
+Masimulizi mawili
Simulizi la kwanza: „Siku moja Yesu …“ Marko 12: 41 – 44 katika rika zote.
Kujenga „daraja“ katikati ya somo la kwanza na pili: Bila shaka sisi tungemsifu mtu aliyetoa fedha nyingi, lakini Yesu alionyesha kwamba mwanamke yule alitoa zaidi kuliko matajiri wale, kwa sababu alimpa Mungu vyote alivyokuwa navyo na hawa walikuwa na vingi vilivyobaki katika mifuko yao.
Mwanamke wa somo la pili alifanya tendo zuri sana kwa Yesu. Na Yesu alifurahi kupata tendo hili lakini wanafunzi wake hawajaelewa vizuri huyu mwanamke na matumizi ya fedha zake. Tusikie somo lingine la mwanamke ambaye alitoa fedha kwa moyo wake na alipata changamoto gani na wanafunzi wa Yesu.
- Simulizi la pili: “Yesu anapakwa marashi” kuhusu Johana 12: 1 – 8 44 kwa rika zote.Siku nyingine, karibu na sherehe ya Pasaka, Yesu aliwatembelea marafiki zake Lazarao na Mariamu pamoja na wanafunzi wake. Walikaa pamoja halafu hii hiki kiliotkea……
Picha B inayohusiana na somo Yohana 12: 1 – 8
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Kwa somo la kwanza (uonyeshe tena picha ya somo la kwanza): Yesu alikuwa wapi na alikaa wapi?
- Alifanya nini?
- Mama mjane alipofika alifanya nini?
- Kwa nini Yesu alimsifa sana kuliko matajiri?
- Kwa somo la pili (uonyeshe picha ya somo la pili): Thamani ya zawadi ya Mariamu ilikuwa kiasi gani?
- Yesu alisema nini juu ya wanawake hawa?
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Kwa somo la kwanza (uonyeshe picha ya somo la kwanza): Yesu na wanafunzi wake wake walikuwa wapi?
- Alifanya nini hekaluni, sehemu ya wanawake?
- Thamani ya sadaka ya mjane ilikuwa kiasi gani?
- Kwa nini alitoa fedha zake zote?
- Kwa nini Yesu alimsif sana?
- Aliona nini ndani ya moyo wake?
- Kuhusu somo la pili: Huyu mwanamke wa pili (uonyeshe picha ya somo la pili) alifanya nini?
- Thamani ya zawadi ya Mariamu ilikuwa kiasi gani?
- Ni nani aliyekasirika alipoona matendo ya Mariamu? Kwa sababu gani?
- Yesu alisema nini juu ya wanawake hawa?
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Kwa somo la kwanza (uonyeshe picha ya somo la kwanza) Yesu na wanafunzi wake wake walikuwa wapi?
- Alifanya nini hekaluni, sehemu ya wanawake?
- Thamani ya sadaka ya mjane ilikuwa kiasi gani?
- Kwa nini alitoa fedha zake zote?
- Kwa nini Yesu alimsifu sana?
- Aliona nini ndani ya moyo wake?
- Kuhusu somo la pili: Huyu mwanamke wa pili (uonyeshe picha ya somo la pili) alifanya nini?
- Thamani ya zawadi ya Mariamu ilikuwa kiasi gani?
- Ni nani aliyekasirika alipoona matendo ya Mariamu? Kwa sababu gani?
- Yesu alisema nini juu ya wanawake hawa?
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Msatri wa moyo ni kutoka kitabu cha 2. Wakorintho 9: 7b na unasema: “Maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Mungu anampenda nani?
- “Ukunjufu” ni nini?
- Ukitoa kwa moyo wa ukunjufu unajisikiaje?
- Je, unaweza kutoa kitu gani na kumpa mtoto mwingine au Mungu?
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kutumia wimbo. Utunge sauti yaa mstari wa moyo huo kwaa maneno yale yale.
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Msatri wa moyo ni kutoka kitabu cha 2. Wakorintho 9: 7b na unasema: “Maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa kati:
- Mungu anampenda nani?
- “Ukunjufu” ni nini?
- Ukitoa kwa moyo na ukunjufu unajisikiaje kuliku ukitoa kwa sababu ulilazimishwa?
- Je, kitu gani kinaweza kutolewa na wewe na kumpa mtoto mwingine au Mungu? Uongee na jirani yako kuhusu swali hili.
- Kitu gani kimetolewa kutoka kwetu na kuwapa watoto wengine? Au tunmetoa kitu gani nakuwapa watoto wengine?
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Msatri wa moyo ni kutoka kitabu cha 2. Wakorintho 9: 7b na unasema: “Maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Mungu anampenda nani?
- “Ukunjufu” ni nini?
- Ukitoa kwa moyo na ukunjufu na ukitoa kwa sababu ulilazimishwa? Unajisikiaje?
- Je, kitu gani kinaweza kutolewa na wewe na kumpa mtoto mwingine au Mungu? Au je, unaweza kutoa kitu gani cha kumpa mtoto mwingine au Mungu?
Uongee na jirani yako kuhusu swali hili. Mpate vitu vitano ambavyo ninyi mtaweza kutoa na kuwapa watoto wengine.Kitu au jambo gani la pekee wewe unaweza kumpa Mungu? Ukumbuke jibu lako kwa sababu baadaye tutalihitaji tena!
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Baadaye wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au katika nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na masomo haya kuhusu „Tutoe kwa moyo.“ Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto watafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisi kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).