+Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watajifunza mazingira ya harusi ya kipindi cha Yesu kwa kupitia mfano wa Yesu wa “Wanawali kumi”.
- Watatambua tofauti ya wasichana wapumbavu na wasichana wenye roho nzuri na busara.
- Watatiwa moyo kujiweka tayari kwa wakati atakapokuja Bwana Yesu na kujenga Imani yao.
+Maelezo juu ya somo
Yesu alitoa mfano huu katika nyakati zake za mwisho, siku chache kabla ya sherehe ya Passach. Alipenda wanafunzi wake tayari kumpokea tena atakaporudi kwake.
Tunahitji kuangalia tamaduni za harusi kwa kipindi kile cha Yesu. Katika harusi ya Wayahudi karamu ya harusi ililfanyika jioni, baada ya siku nzima ya kuchezecheza na shamrashamra nyingine. Mwisho wa siku huyu bwana harusi alichukuliwa na marafiki zake kwa ajili ya kwenda katika maandamano mpaka nyumbani kwa wazazi wa bibi harusi. Anafika kabisa nyumbani kwake. Bwana harusi na marafiki zake wanapokelewa na wanawali, yaani wampambe bibi harusi. Kwa njia hii bwana harusi na kikundi chake wanatangaza harusi hii. Kutoka na tamadunii za kiyahudi ilikuwa muhimu kabisa kutimiza wajibu wao kwa pande zote mbili: Bwana harusi na kikundi chake na bibi harusi na wanawali. Lakini bibi harusi na wanawali hawajua kabisa muda wa kufika bwana harusi. Wakati huo haukujulikana kabisa. Muhimu tu ni bibi harusi na wanawali wako tayari na bibi harusi ameshapambwa na wanawali.
Jioni ya kufika kwa bwana harusi ni ndani ya siku kumi ya sherehe. Ndani ya siku hizi bibi harusi na wanawali wamemjua tu bwana harusi na kikundi chake wanakuja. Kama bibi harusi na wanawali wakisikia bwana harusi na marafiki zake wakiingia sehemu ya wazazi wa bibi harusi wanawali wanaenda njje na bwana harusi anapokelewa kwa heshima na furaha. Wanamsindikiza mpaka nyumbani kwa bibi harusi kumchukua. Wote wanatembea sasa kwa maandamano kwenda nyumba ya bwana harusi. Na nyumbani kwake sherehe ya harusi inaanza sasa. Katika sherehe hii wanakijiti wanakaribishwa wote wa kijijini kwa harusi hii maana ndugu, marafiki na majirani.
Ukimpokea bwana harusi nje katika gizani ni lazima tuwashe koroboi. Kwa hiyo ni bora usafishe kamba ya koroboi kabla ya kuwacha ili ilete koroboi inaleta mwanga zaidi na wa kutosha.
Ndani ya mfano huu wasichana watano wanatumia mafuta yote mwanzoni wakati wa kumsubiri bwana harusi. Wasichana wengine watano wanalala kwanza na kama wakisikia bwana harusi anaingia mazingira ya bibi harusi wanaonyesha wako tayari kumpokea kwa mwanga wa koroboi, furaha na utayari kutoka moyoni mwao.
Wasichana wenye busara walilala kwanza na kutumia mafuta kwa umakini. Wanaonyesha wako tayari kutunza na kujenga Imani yao. Ndani ya mfano huu koroboi ni picha ya Imani yetu, hasa mafuta ya koriboi. Kamba ya koroboi ni kama moyo wa mtu. Kama usingesafisha kamba ya koroboi usingefaulu kuwasha koroboi vizuri ili ignae na mwanga wake. Usingesafisha moyo wako mara kwa mara usingeweza kumpokea bwana harusi/Bwana Yesu. Mafuta ndani ya koroboi ni Imani ya watu. Imani ya watu inawaka vizuri kama moyo uko safi. Sisi tuwe tayari kusafisha mioyo yetu kila wakati ili tuweze kumpokea Bwana Yesu.
Kitu kingine: Imani huwezi kumpa mtu mwingine kwa hiyo wasichana wenye busara hawawezi kuwapa wasichana wapumbavu mafuta yao, kwa sababu kila mtu ana imani/mafuta yake.
Pia imani yetu inapungua muda fulani na inaongezeka kipindi kingine kama mafuta ndani ya koroboi.
Yesu anapenda tuwe tayari, tusafishe mara kwa mara mioyo yetu, tuwe makini ndani ya imani yetu. Kwa hiyo alifurahahishwa wasichana wenye busara waliotunza mafuta yao badala kutumia ovyo ovyo.
Katika mfano huu wasichana wale waliomngojea bwana harusi ni mfano wa kanisa linalongoja kurudi kwake Bwana Yesu katika utukufu wake.
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
- Nani ameshawahi kwenda katika harusi?
- Ukienda katika harusi unahitaji kuandaa nini?
- Bwana Harusi na Bibi Harusi pamoja na kamati wanaandaa nini?
- Ukifanya sherehe ya harusi/kufunga ndoa unapata furaha au faida gani?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi: Leo tunajifunza kuhusu mfano mmoja ambao Yesu alisimulia kuhusu harusi na kitu gani kilichotokea kwao.
+Simulizi
„Siku moja Yesu …“ Mathayo 25: 1 – 13 katika rika zote: Mwanzoni wa simulizi asimulia pia tamaduni za kipindi cha Yesu na wayahudi kuhusu kusherekea harusi na pia kuhusu kutumia koroboi vizuri kwa wakati wa usiku (kusafisha kamba, kuweka mafuta mazuri, kutunza mafuta n.k.).
Uonyeshe picha ya somo la leo!
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Yesu alitumia mfano gani kueleza mambo yake?
- Wasichana wakimsubiri bwana harusi walifanya nini?
- Wasichana waliowasha koroboi walipata changamoto gani?
- Walifanya nini baada ya kuiona changamoto hii?
- Waliporudi kununua mafuta waliweza kuingia katika nyumba ya bwana harusi na kusherekea? Kwa sababu gani?
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Yesu alitumia mfano gani kueleza mambo yake?
- Wanawali wakimsubiri bwana harusi walifanya nini?
- Wasichana waliowasha koroboi walipata changamoto gani?
- Tunaweza kusema wao ni wasichana wa namna gani?
- Walifanya nini?
- Waliorudi kutoka dukani kununua mafuta waliweza kuingia katika harusi na kusherekea? Kwa sababu gani?
- Kwa nini wengine watano waliingia katika sherehe vizuri?
- Wasichana gani walionyesha busara na wasichana gani walionyesha ubumbavu?
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Yesu alitumia mfano gani kueleza mambo yake?
- Wanawali wakimsubiri bwana harusi walifanya nini?
- Waliposikia kwamba bwana harusi anakuja, wote walifanya nini?
- Kwa nini wenye busara hawakuweza kuwasaidia wenzao wasiokuwa na mafuta?
- Ilitokea nini kwa wasichana waliokuwa alipokuja bwana harusi?
- Waliporudi kutoka madukani wale wapumbavu walipata nini?
- Kwa nini Yesu anasema wasichana wengine ni wapumbavu na wasichana wengine ni wenye busara?
Maelezo mafupi kwa watoto wa umri wa kati na wakubwa:
Ndani ya mfano huu tunaona
- Wasichana kumi
- Bwana harusi na
- Koroboi
- Wasichana ni picha yetu: Sisi tunamwamini ya Mungu. Na sisi ni wanashiriki.
- Namba kumi inamaanisha, kama vidole kumi vyote au kama amri kumi zote.
- Bwana harusi ni Bwana Yesu ambaye atakuja tena duniani.
- Koroboi ni picha ya imani yetu.
Tuangelie koroboi na imani yetu. Picha ya koroboi: Koroboi ni chombo ambacha kinawekwa mafuta na kamba katikati. Tukikiwasha kamba mafuta yanapandisha juu, kamba inawashwa na ina ulimi wa moto. Ulimi wa moto unaleta mwanga na unapunguza giza.
Lakini ni muhimu huyu ambaye ana koroboi ajue kutumia vizuri:
- Atunze koroboi
- Asafishe kamba mara kwa mara
- Aangalie kama mafuta yameisha au yanatosha.
- Awashe koroboi, alete nuru ili aweze kumpokea mtu/bwana harusi kwa kipindi cha giza.
Kama koroboi ni imani, je inanmaanisha nini kwetu?
Koroboi ni kama mwili wetu, kamba ni kama moyo wetu, mafuta ni kama imani yetu. (Uangalie picha tena!)
Tukiangalia utunzaji mzuri wa koroboi unatueleza mambo manne pia katika imani yetu.
- Tutunze mwili wetu vizuri kama koroboi.
- Tusafishe moyo wetu mara kwa mara kutoa uchafu na dhambi.
- Tuangalie mara kwa mara imani yetu kama imepungua na sisi hatuna nguvu au imani inayotosha na kuongezeka kiasi cha kushinda giza katika maisha yetu.
Giza katika maisha yetu ni kama hofu, mashaka, maneno mabaya, dhambi, magonjwa, kifo n.k. Tukikaa mbali na Mungu tutapata shida hizi. Imani inapungua kwa haraka.
- Uweke moyo wako, uwe tayari kun`gaa ili uweze kumpokea Bwana harusi/Bwana Yesu.
Wasichana wenye busara walijua kuwasha koroboi yaani moyo wao kwa muda gani na walitunza koroboi na miili yao kwa kulala kidogo. Walisafisha kamba ili koroboi inan`gaa zaidi. Kwa hiyo walishika imani yao na kuwa karibu na Mungu. Hii ndiyo sababu iliyowafanya waingie katika sherehe ya harusi.
Wasichana wapumpavu waliishiwa na mafuta maana ni walipungukiwa imani yao kwa kutumi mafuta mapema. Labda walipata hofu gizani au walipato hofu watachelewa kumpokea bwana harusi. Kwa hiyo waliwasha kamba ya koroboi. Maana ni hawajatunza moyo wao vizuri kwa sababu yahofu, mashaka au mambo mengine yameingia. Walipotafuta mafuta (Imani) wamepoteza muda na hawaruhusiwi kuingia katika sherehe ya harusi tena. Wamepoteza mwelekeo wa imani ya wayahudi na wakristo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Luka 11:28 na unasema: “Lakini heri zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kilishika.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Nani anapata heri?
- Anahitaji kufanya nini?
- Unalisikia Neno la Mungu wapi?
- Unalishika Neno la Mungu wapi? (moyoni na kichwani)
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kupita isahara inayoelezwa:
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Mathayo 24:42 na unasema: „ Kesheni basi, kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”
Maswahli kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati:
- Tukeshei kwa sababu gani?
- Kama Bwana atakuja tena tufanye nini?
- Tunaweza kujiandaa kwa njia gani kumpokea vizuri?
- Kwa nini Yesu anawambia wanafuzi wake mfano huu kabla ya kifo chake?
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye wauandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Mathayo 24:42 na unasema: „Kesheni basi, kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.”
Maswahli kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa kubwa:
- Tukeshei kwa sababu gani?
- Kama Bwana atakuja tena tufanye nini?
- Tunaweza kujiandaa kwa njia gani kumpokea vizuri?
- Kwa nini Yesu anawambia wanafuzi wake mfano huu kabla ya kufa kwake?
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo. Halafu wachore picha inayoonyeshwa na watoto wakubwa chini ya maandiko yao. Wakitumia ukurasa mdogo wachore picha nyuma ya ukurusa huu!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na somo hili la mfano wa wanawili. Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto wanafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).