+Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watafahamu kuwa Mungu husikia maombi ya watu wanaomjia kwa unyenyekevu, uaminifu, ukweli utaratibu na amani.
- Watagundua kama Farisayo na mtoza ushuru wanatumia njia ya nzuri na mbaya ya kuomba kwa namna hii wanapoongea na Mungu.
- Wataelewa tuna njia mbalimbali za kumwombeaMungu (kumtii Mungu, kumshukuru, kumwambia makosa yetu, kumwomba Mungu kwa huruma zake na atuonee,)
- Watamwomba Mungu kwa kutubu makosa yao na kupokea msamaha wa Mungu.
+Maelezo juu ya somo
Katika Nchi Takatifu watoza ushuru walichukizwa sana wakati wa Agana Jipya. Walikuwa wakifanya kazi kwa ajili ya serikali ya kirumi, tena waliwanyang’anya watu na kuchukua sehemu kubwa na kuiweka katika mfuko wao wenyewe.
Mafarisayo waliheshimiwa sana na watu kwa jinsi walivyomcha Mungu na kujitahidi kizitimiza sheria zake. Wengi walikuwa wema lakini ilikuwa rahisi kwao kujivuna kama mtu huyu katika habari hii.
Huyu mfarisayo ndani ya mfano huu anaonyesha njia nzuri ya kumtii Mungu na kufuata sheria za Mungu. Anafunga mara mbili kwa wiki, anatoa zaka sehemu ya kumi ya pato lake n.k.. Lakini shida yake ni jinsie anavyomwomba Mungu na kumshukuru ni kwa kujivuna na kujisifu.
Mtoza Ushuru anatumia maneno machache tu:”Ee, Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.“ (Luka 18:13)
Ndani ya somo hili tunaweza kujifunza mambo matano ya maombi:
- Tumtii Mungu kama Mafarisayo
- Tumshukuru Mungu kama Mfarisayo
- Tumwambie makosa yetu kama Mtoza Ushuru
- Tumwombee Mungu atuonee hurumu na atusamehe makosa yetu.
- Tuombe kwa njia ya unyenyekevu, uaminifu, ukweli, utaratibu na amani.
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
- Nani ameshawahi kumwona mtu/mtoto anayejisufu na kujivuna?
- Watu wakifanya hivi watakuwaje?
- Watu wanaojisifu na kujivuna wanapata changamoto gani ndani ya jamii na uhusiano?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi katika rika zote: Leo tunajifunza kuhusu mfano mmoja kutoka kwa Yesu na changamoto ndani ya mfano huu kwa watu wawili ambao wanaomba sala tofuati sana. Tusikie mfano wa Yesu na tabia ya mtu gani Yesu anaipenda sana.
+Simulizi
„Siku moja Yesu …“ Luka: 18: 9 – 14 katika rika zote
Uonyeshe picha ya somo la leo!
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Walikuwa watu gani waliopanda kwenda hekaluni kusali?
- Farisao alisali nini?
- Mtoza ushuru aliomba nini kutoka kwa Mungu?
Maelezo mafupi: Mmojawapo alimshukuru Mungu na mwingine alimwomba Mungu kupata huruma ya Mungu kwa sababu alifanya matendo mabaya. (Dhambi watoto wanaelewa kiasi tu. Utumie maneno ya „matendo mabaya“)
Tunaweza kumshukuru Mungu, kumwomba jambo au mtu kumwambia Mungu kwamba tumefanya matendo mabaya.
Vitendo vinafanywa pomoja: Wanasali pamoja kwa kutumia alama za aina tatu ya kusali!
Maua: alama ya kumshukuru au kumsifu Mungu kama Farisayo
Mshumaa mdogo: alama ya kumwomba Mungu kama Mtoza ushuru
au kibiriti kimoja: kupata mwanga kwa maisha na imani yetu
Jiwe dogo : alama ya kumwonyesha Mungu kwamba tumekosa; tunabeba mzigo (dhambi au matendo mabaya) kama jiwe juu ya moyo wetu.
Watoto wadogo wakusanyanike katika duara. Labda wanakaa katika viti au chini ya mkeka. Katikati yao ni stuli na msalaba kwa ajili ya alama ya Yesu. Alikufa kwa ajili yetu ili tupate uhai na uhuru kwa sababu alichukua dhambi zetu.
- Kila mtoto anachagua kitu kimoja kama jiwe, kibiriti kimoja, mchumaa mdogo au ua. Afanye sala yake na maneno yake.
- Akilichugua ua anamshukuru Mungu: „Mungu nakushukuru kwa ….!“
- Akichugua mchumaa mdogo au kibiriti kimoja amwambie Mungu: „Mungu, Baba nakuomba kwa …!“
- Akilichugua jiwe amwambie Mungu alikosa kwa tendo gani: „Mungu, unisamehe. Nilikosa kwa kufanya ….!“
- Wafanye sala hii pamoja kwa kutumia alama mojawapo pamoja na sentensi yake.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Walikuwa watu gani waliopanda kwenda hekaluni kusali?
- Farisayo alisali nini?
- Alifanya uzuri gani?
- Alifanya kosa gani ndani ya sala yake?
- Mtoza ushuru aliomba nini kwa Mungu?
- Alisema nini?
- Huyu Farisayo alifanya nini kizuri ndani ya sala yake?
- Nani kati ya wao alifanya vizuri? Kwa sababu gani?
- Kwa hiyo Yesu anapenda tutumie njia gani tukisali?
Maelezo mafupi: Farisayo alimshukuru na kumsifu Mungu na hili alifanya vizuri. Lakini alijisifu na kujivuna sana. Hii kweli ni vibaya. Alipenda sana kufuata njia ya sheria na kumfuata Mungu. Na kweli anafanya kwa matendo mengi. Lakini alikosa alipoanza kujisifu na kujivuna.
Mtoza Ushuru alimwombia Mungu “Unihurumie!” Alijua alikosa kwa hiyo alitubu kosa lake.
Kwa hiyo Mungu anapenda sisi tutumie njia ya unyenyekevu, uaminifu, ukweli, utaratibu na amani tukisali.
Tukisali tunaweza kutumia njia tano mbalimbali: Tunaweza
- Kumshukuru Mungu
- Kumsifu Mungu
- Kumwomba Mungu kwa jambo fulani au mtu
- Kumwambia kosa letu na kutubu makosa
- Kumwomba Mungu aturehemu na kutusamehe
Leo tunamshukuru Mungu au tumsifu Mungu kwa jambo moja lakini pia tunamwambia makosa yetu:
- Watoto wote wasimame kwa nusu duara mbele ya madhabahu. Waseme kwanza wanamsifu au wanamshukuru Mungu kwa jambo gani? Halafu wote wapige magoti kwa sababu wanatubu makosa yao kwa unyenyekevu na ukweli. Mwishoni wote tumwombe Mungu pamoja: „Mungu utusamehe! Mungu uturehemu!“
- Mwalimu ashike mkono wa kulia ili awasaidie kusimama tena. Wakisimima amwambie kila mtoto: „Mungu amekusamehe!“. Asema sentensi hii achore msalaba na kidole chake ndani ya mkono wao.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Walikuwa watu gani waliopanda kwenda hekaluni kusali?
- Farisayo alisali vipi?
- Alifanya kitu gani kizuri?
- Na alifanya kosa gani ndani ya sala yake?
- Mtoza Ushuru aliomba nini kwa Mungu?
- Alisema nini?
- Huyu Farisayo alifanya nini kizuri na nini kibaya ndani ya sala yake?
- Nani kati yao alifanya vizuri kuliko mwingine? Kwa sababu gani?
- Kwa hiyo Yesu anapenda tusali kwa njia gani?
Maelezo mafupi: Farisayo alimshukuru na kumsifu Mungu na hili alifanya vizuri. Lakini alijisifu na kujivuna sana. Hii kweli ni vibaya. Alipenda sana kufuata njia ya sheria na kumfuata Mungu. Na kweli anafanya kwa matendo mengi. Lakini alikosa alipoanza kujisifu na kujivuna.
Mtoza Ushuru alimwomba Mungu “Unihurumie!” Alijua alikosa kwa hiyo alitubu kosa lake.
Kwa hiyo Mungu anapenda kutoka sisi tutumie njia ya unyenyekevu, uaminifu, ukweli, utaratibu na amani tukisali.
Tukisali tunaweza kutumia njia tano mbalimbali: Tunaweza
- Kumshukuru Mungu
- Kumsifu Mungu
- Kumwomba Mungu kwa jambo fulani au mtu
- Kumwambia kosa letu na kutubu makosa
- Kumwomba Mungu aturehemu na kutusamehe
- Leo tunamshukuru Mungu na kumsifu Mungu kwa jambo moja lakini pia tunamwambia makosa yetu.
- Watoto wakubwa waandike kwa upande mmoja wa ukurasa mdogo makosa yao matutu waliyofanya wiki ilyopita.
- Baada ya hili watoto wote wasimame kwa nusu duara mbele ya madhebahu. Waseme kwanza wanamsifu au wanamshukuru Mungu kwa jambo gani? Halafu wote wapige magoti kwa sababu wanatubu makosa matatu yao kwa unyenyekevu na ukweli. Mwishoni wote tumwombe Mungu pamoja: „Mungu utusamehe! Mungu uturehemu!“
- Mwalimu ashike mkono na kulia awasaidie kusimama tena. Wakisimima awambie kila mtoto: „Mungu amekusamehe!“. Asema sentensi hii achore msalaba na kidole chake ndani ya mkono wao.
- Mwishoni kabisa watoto waandike sentensi ya “Mungu utusamehe! Mungu uturehemu!” katika upande mwingine wa ukurasa mdogo. Wachore maua mazuri pembeni ya sentensi hizi kuonyesha Mungu wamefurahi sasa kwa sababu aliwasamehe.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Zaburi 86:5a na b na unasema: “Kwa maana wewe, Bwana U mwema. Umekuwa tayari kunisamehe.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Mungu ni mwema kwa kitu gani?
- Pia Mungu yupo tayari kufanya nini?
Maelezo mafupi: Mungu ni tayari kutusamehe kwa sababu sisi tunaongea naye ndani ya sala.
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kutumia wimbo. Upate sauti nzuri ya maneno haya ya mstari wa moyo. Uimbe mara tano wimbo wa mstari wa moyo na watoto wadogo. Utumie kweli maneno yale yale ya mstari wa moyo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Zaburi 86:5 na unasema: “Kwa maana wewe, Bwana U mwema. Umekuwa tayari kunisamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao.”
Maswahli kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati (ya miaka 7 – 9):
- Mungu anatupa wema gani kwa kitu gani?
- Mungu pia yupo tayari kufanya nini?
- Kwa sababu gani anafanya yote haya kwetu?
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Zaburi 86:5 na unasema: “Kwa maana wewe, Bwana U mwema. Umekuwa tayari kunisamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao.”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wakubwa:
- Mungu anatupa wema gani kwa kitu gani?
- Mungu pia yupo tayari kufanya nini?
- Kwa sababu gani anafanya yote haya kwetu?
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au kwa ukurasa mdogo. Halafu wachore picha inayoonyeshwa na watoto wa umri kati chini ya maandiko yao. Wakitumia ukurasa mdogo wachore picha kwa nyuma ya ukurusa huu!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na somo hili kuhusu sala na maombi . Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto wanafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).