+Malengo ya Somo
Kupitia somo hili watoto
- Watafahamu kuwa Mungu anatupa sisi sote nafasi ya kusikia Neno lake.
- Wataelewa kwamba watu wanasikia Neno la Mungu kwa njia tufauti (kwa kichwa tu au kwa moyo).
- Watakuwa tayari kutii katika maisha yetu kwa sababu wamevutwa kupokea wakovu.
+Maelezo juu ya somo
Utangulizi (mazungumzo) katika rika zote
- Nani ameshawahi kumwona mkulima au mpanzi?
- Mkulima au mpanzi anafanya kazi gani?
- Huyu anapata changamoto gani na kazi yake?
Kujenga „Daraja“ kati ya utangulzi na simulizi katika rika zote: Leo tunajifunza kuhusu mfano mmoja wa Bwana Yesu kuhusu mpanzi/mkulima. Huyu mpanazi alipata changamoto fulani alipopanda mbegu zake. Changamoto gani na nini kilichotokea kwa kazi hii tunasikia sasa.
+Simulizi
„Siku moja Yesu …“ Marko 4: 1 – 9 katika rika zote
Watoto waangalie pia picha kuhusu somo hii, hasa mstari wa 1 hadi 9.
Picha inayohusiana na somo Marko 4. 1 – 9
Ukiwafundisha watoto wadogo uishie hapa mstari wa 9. Ukisimulia zaidi ni mambo mengi kwao.
Ukiwafundisha watoto wa ya kati au watoto wakubwa uendele na somo: mstari wa 10 mpaka 20.
Simulizi linaenelea katika mstari wa 10 hadi 20:
„Yesu aliwasimulia mfano mmoja kuhusu mpanzi mmoja na changamoto yake. Wanafunzi walitatanishwa sana baada ya kusikia mfano huu. Walijiuliza “Yesu anapenda kusema nini? Mbegu,
Mwalimu Ingrid Walz, Mafundisho ya Shule ya Jumapili 2
udongo unamaanisha nini? Huyu mpanzi ni nani? Na pia mawe, jua miamba vinawakisha inakaa kwa mambo gani?“
Kwa hiyo walimwomba Yesu aendelee kuezelza mfano wake. … Kuendelea na mistari 13 – 20
Wameanza kuelewa kwa taratibu na wanaanza kujiuliza tena: „Mimi ni kama udongo wa namna gani? Moyo wangu unasikia Neno la Mungu au ni masikio tu? Je, ninakuwa kama udongo wa nne nitaleta mazao mengi?“
Kila mwanafunzi alianza kufikia zaidi kuhusu mfano huu. “
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Mpanzi alifanya nini?
- Mbegu zimeanguka wapi na wapi?
- Nini limechotokea ikawa mbegu zimerushwa katika miamba, miiba au njiani?
- Kama jua ni kali kitu gani kinachotokea kwa mbegu?
Maelezo mafupi: Mwalimu anajumlisha majibu ya maswali: Kwa hiyo tunaweza kusema kwamba mpanzi alizirusha mbegu zake, lakini mbegu zimeanguka kwa katika sehemu nne tofauti. Kwa mfano kwa njia, katikati ya miiba au juu ya miamba. Jua pia limeziunguza mbegu. Lakini mbegu nyingine zimeanguka katika kwa ardhi nzuri na zimetoa mazao mengi sana.
Sasa sisi tunafanya vitendo kuhusu kukua na mbegu:
Tulale chini kama mbegu, tunajikunjua, tunajibua, tunakua na kukua mpaka tuwe warefu sana. Tunatoa mazao. Safi sana. Tufanye tena, na mara ya tatu.
Sasa tunafanya tena, lakini tunaangalia nini inatusumbua kwa kukua kwetu. Jua ni kali na sisi tunainama. Miamba inatusumbua kwa sababu tunaona inaituumiza. Kwa mawe hatuweza kupata mizizi mizuri. Kwa hiyo tunajumbajumba kwa sababu ya upepo. Tunaweza pia kuanguka kwa sababu hatuwezi kusimima vizuri. Hakuna mizizi na mizizi ni kama miguu ya mimea.
Watoto na mwalimu wanajaribu njia ya mbalimbali katika kukua katika shida fulani kama kukua chini ya jua kali, au bila mizizi au katikati ya miiba na miamba.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Yesus alitumia mfano gani kueleza mambo kuhusu Neno la Mungu? Utueleze kwa kifupi!
- Ndani ya mfano huu kila kitu kina maana. Je, unafikiri maana ya mpanzi ni nini?
- Au mpanzi ni nani?
- Mbegu ni nini?
- Udongo unamaanisha nini?
- Kama msingi wa kukua ni tofuati utapata mazoa aina gani?
Maeelzo mafupi: Tukitafsiri leo, tunaweza kusema kila msingi wa kukua ni tofauti. Maana ni kila moyo wa kulipokea Neno la Mungu ni tofauti. Wengine wanasikia Neno la Mungu lakini wanasahau tena kwa haraka. Mambo mengi yanaingia kama miimba kwa mimea.
Wengine wanasikia tu Neno la Mungu lakini Neno la Mungu halishuki mpaka moyoni mwao. Kwa hiyo ni kama Neno la Mungu linarushwa kwa mawe, mwamba au miamba. Neno la Mungu haliwezi kupata mizizi ndani ya moyo wa wasikilisaji.
Wengine wanapokea kwa moyo lakini marafiki, ndugu au watu wengine wanawambia kitu kibaya tena. Huyu aliyeliamini Neno la Mungu anapata mashaka, hofu au chagamoto kuliamini tena. Ni kama Neno la Mungu limerushwa njiani. Na ndege wanakuja kuchukua mbegu (Neno la Mungu) tena na tena. Kwa sababu wanaikula mbegu za mpanzi.
+ Maswali na mazungumzo kuhusu somo la leo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Mpanzi alizirusha mbegu zake. Lakini hawezi kupata kila sehemu mazoa mazuri. Kwa sababu gani?
- Kwa hiyo vitu vyingi ndani ya mfano huu vinakuwa kama picha kwa kueleza vitu vyingine. Mpanzi ni nani? Mbegu ni nini? Udongo ni nini? Maana ya jua, miamba, mawe, njia ni nini?
- Yesu anatumia mfano huu na anaeleza jua, miamba, miiba, mawe na njia vimeleta changamoto kwa mbegu kujibua au kukua. Anapenda kueleza nini kwa kutumia picha hizi kuhusu kukua ndani ya imani?
Mazelezo mafupi: Siku hizi sisi hatuwezi kupata Neno la Mungu moja kwa moja kutoka kwa Yesu. Yesu ameshafufuka na alirudi mbinguni. Sasa
tunalipata Neno la Mungu linapatikana wapi na kwa njia gani? Unafikiri kwa njia gani tunalipata Neno la Mungu?
- Wengine wanaenda kanisani na Shule ya Jumapili kwa ajili ya kulisikiliza Neno la Mungu
- Wengine wanafurahi kupata ujumbe kutoka kwa Mungu ndani ya maombi yao.
- Wengine wanalisoma Neno la Mungu kila siku kutoka katika Biblia zao.
Tukipenda kujua Neno la Mungu zaidi na zaidi tunahitaji kufanya mambo yote. Lakini kwanza ni muhimu kujua mambo zaidi kuhusu Biblia.
Leo tuanagelie Biblia zaidi:
- Biblia ina sehemu gani kubwa?
- Zinaitwaje?
Tuna Agano la Kale na Agano Jipya.
Ndani ya Agano la Kale tunaweza kujifunza na kusoma mambo ya
i.) Kihistoria/historia ya watu wa Mungu: Waisraeli na Wayahudi.
ii.) Sheria, walizopewa kutoka kwa Mungu.
iii.) Maelezo na hotuba za manabii waliowaita watu wamwabudu Mungu kwa moyo na kweli.
iv.) Nyimbo za kumsifu Mungu zipo katika vitabu vya Mashairi.
Jumla tuna vitbabu 39 kwa Agano la Kale.
Kwa Agano Jipya tunaweza kusomo kuhusu
i.) Kwake Bwana Yesu (vitabu hivi vinaeleza jinsi ahadi ya Agano la Kale vilivyotimizwa katika maisha, kifo na kufufuka kwake Yesu.)
ii.) Pia vinaeleza jinsi kanisa lilivyoendelea na kazi ile ile ya kuwavuta watu kumtumikia Mungu wa kweli.
Katika Agano Jipya kuna vitabu 27 kwa jumla.
Mchezo wa mashindano kwa watoto wakubwa: Watoto wakubwa wanaambiwa mistari fulani kutoka Agana la Kale na Agano Jipya. Wanaifungua kwa haraka na huyu ambaye aliifungua na kuipata mstari huu kwa kwanza ameshinda. Uifatilie mistari mitano mpaka kumi na watoto wana Biblia wanaweza kushiriki ndani ya mchezo huu.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wadogo, miaka 4 - 6
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Yakobo 1:21b na unasema: “…jiwekeni chini ya Mungu na kupokea lile neno nililolipandwa mioyoni mwenu!”
Maswali kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wadogo:
- Mungu anapenda tufanye nini?
- Nini alipanda ndani ya moyo wetu?
- Moyo wetu ni kama kitu gani kutokana na mfano wa Yesu?
4. Watoto wadogo wakariri mstari wa moyo kwa kupita ishara zinazoelezwa:
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo.
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wa kati, miaka 7 - 9
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka ktiabu cha Yakobo 1:21b na unasema: “…jiwekeni chini ya Mungu na kupokea lile neno nililopandwa mioyoni mwenu, ambalo laweza kuziokoa nafsi zenu!”
Maswahli kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wa umri wa kati:
- Mungu anapenda tufanye nini?
- Mungu alipanda nini ndani ya moyo mwetu?
- Moyo mwetu ni kama kitu gani kutoka mfano wa mpanzi ambao Yesu alisimulia?
- Na Neno la Mungu linaweza kufanya nini kwa nafsi zetu?
4. Watoto wa umri wa kati wakariri mstari wa moyo. Baadaye waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo na wachore picha inayofuata chini ya maandiko au nyuma ya ukurasa mdogo!
5. Watoto waelewe Mstari wa Moyo
+ Mstari wa Moyo kwa watoto wakubwa, miaka 10 - 12
- Watoto wausikie Mstari wa Moyo.
- Watoto wauone Mstari wa Moyo. Uandike Mstari wa Moyo ubaoni! Wanaoweza kusoma wasome katika Biblia.
- Watoto wazungumzie kuhusu Mstari wa Moyo.
Mstari wa moyo ni kutoka kitabu cha Yakobo 1:21b na unasema: “…jiwekeni chini ya Mungu na kupokea lile neno nililopandwa mioyoni mwenu, ambalo laweza kuziokoa nafsi zenu!”
Maswahli kuhusu mstari wa moyo kwa watoto wakubwa:
- Je, unapata faida gani ukiyajua maandiko matakatifu?
- Tangu kipindi gani maanadiko yanasema unalikumbuka Neno la Mungu?
- Unahitaji nini kupata wokovu wa Mungu?
- Unafikiri mstari huu una uhusiano gani na mfano wa mpanzi ambao Yesu alitusimulia leo?
4. Watoto wakubwa wakariri mstari wa moyo. Waandike mstari wa moyo katika madaftari yao au katika ukurasa mdogo. Halafu wachore picha inayoonyeshwa na watoto wa umri wa kati chini ya maandiko yao. Wakitumia ukurasa mdogo wachore picha kwa nyuma ya ukurusa huu!
5. Watoto waelewa Mstari wa Moyo.
+ Wimbo
Mwisho wa mafundisho unaimba wimbo unaoendana na somo hili kuhusu sala na maombi . Kama ukiweza utunge mwenyewe. Watoto wanafurahi kuimba somo au mstari wa moyo.
+ Kurudi darasani
Pia watoto wote wakutane tena katika darasa lenye madhabahu au mbele ya kanisani kwa ajili ya kumaliza ibada ya watoto.
6. Watoto warudie mstari wa moyo mwishoni tena ndani ya liturgia, baada ya Sala ya Bwana na kabla ya Utume (baraka za Mungu).